PICHA ZOTE ZINAONYESHA NAMNA CPB INAVYOCKAHATA NA KUFUNGASHA MAZAO YA WAKULIMA NA KUYAINGIZA SOKONI |
NA JOYCE KASIKI,MBEYA
MKURUGENZI wa Bodi ya Nafaka ya Mazao Mchanganyiko (CPB) Dkt.Anselm Moshi amesema,Bodi hiyo inaendelea kujenga viwanda vya kuchakata na kuyaongeza thamani mazao ya wakulima kutoka viwanda vinane vilivyopo sasa. Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya wakulima na wafugaji (Nane Nane ) mkoani Mbeya,Mkurugenzi huyo amesema lengo ni kuhakikisha mkulima anakuwa na uhakika wa soko la mazao wanayoyazalisha. Amesema,kutokana na viwanda hivyo ,Bodi hiyo inanunua mazao ya wakulima na kuyaongeza thamani na kuyauza ndani na nje ya nchi. “Tupo katika maonyesho haya kwa ajili ya kutambulisha wakulima bidhaa zetu lakini pia kuwafahamisha wananchi huduma zinazotolewa na CPB ....,napenda kuwahakikishia wakulima masoko ya uhakika ,kwani mpaka sasa tuna viwanda vinane vya kuongeza thamani mazao ya wakulima ambavyo tayari vimeshaanza kufanya kazi lakini pia tunaendelea kujenga viwanda vingine.”amesema Dkt.Moshi Mkurugenzi huyo Amesema,lengo ni kupata viwanda vingi zaidi ili kuwafikia wakulima wote na kuwafanya kuwa na uhakika wa masoko ya kuuza mazao yao. “Kupitia viwanda hivi,tunanunua mazao ya wakulima tunayaongeza thamani halafu tunayauza ndani na nje ya nchi ,hiyo ndio njia ya uhakika ya wakulima kupata masoko ya uhakika .”amesisitiza Mkurugenzi huyo Pia amesema,njia nyingine ya wakulima kupata masoko ya uhakika ni kwa kutumia mtandao mpana wa CPB ambao upo ndani ya nan chi. Kwa mujibu wa Dkt.Moshi ,mtandao huo wa masoko pia upo katika nchi zote za Afrika Mashariki pamoja na Asia na Ulaya ambapo CPB inaendelea kujenga uwezo huo wa kimtandao ili kupata masoko zaidi ya kuuza mazao ndani na nje ya nchi. “Tunataka wakulima na wadau wote wa tasnia ya kilimo wajue kwamba CPB inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusafisha ,kuhifadhi,kupima mazao katika mikoa mbalimbali ikiwemo mikoa ya Arusha,Mwanza,Dodoma na Songwe, Pia tunataka wakulima wajue CPB inazo bidhaa bora na zinaandaliwa kwa umakini na ubora wa hali ya juu ukiwemo unga wa dona,sembe,mchele,mafuta ya kula ya alizeti na mazao mengine kama vile maharage,soya,korosho,asali na dengu. na mazao mengine mengi ambayo bodi inanunua kwa wakulima mbalimbali na kuziandaa na kuzifunhgasha vizuri kwa ajili ya walaji. bidhaa hizo zimesambaa nchi nzima hivyo wananchi wanaweza kuzipata katika vituo hivyo nchi nzima Ninawasa wakulima kutembelea mabanda yetu hapa Nanenane ili waje kujionea wenywe bidhaa hizo Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amesema,Bdi hiyo inaingia mikataba na wafanyabiashara ambapo yenyewe inazalisha na kuyaongeza thamani mazao kwenye viwanda vyake kisha mfanyabiashara anayachukua na kwenda kuuza mwenyewe. Mkurugenzi huyo ametumia nafasi hiyo kuwasihi wakulima ,wafanyabiashara kutembelea banda la CPB ili kujionea shughuli zinazofanywa na Bodi lakini pia waweze kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya kilimo.