Showing posts with label Habari. Show all posts
Showing posts with label Habari. Show all posts

Mhandisi Mramba aipa tano EWURA

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki,Dar Es Salaam


KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati Felichesmi Mramba ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji kwa huduma inayofanya ya udhibiti huku akisema imesaidia kupunguza hata changamoto ya kukatikakatika kwa umeme.

Mramba ameyasema hayo leo Julai 9,2024 kwenye maonesho ya 48 ya  Kimataifa ya Biashara alipotembelea banda la Mamlaka hiyo.

"Leo nimetembelea banda la EWURA, kama mnavyofahamu ,EWURA ni taasisi yenye wajibu wa kudhibiti huduma za Maji na Nishati,kwenye eneo la nishati,tunadhibiti umeme ,huduma za  umeme ,huduma za gesi asilia ,huduma za mafuta,

"Tunachoweza kusema EWURA imefanya kazi nzuri sana mpaka sasa hivi,kama mnavyoona huduma zinazodhibitiwa na EWURA zinapatikana na wameweza kudhibiti upatikanaji wa huduma yenyewe ,bei ya huduma inayotolewa na ubora wa huduma hiyo,sasa kwenye eneo la bei nafikri mnafahamu kwamba nchi yetu ni miongoni mwa nchi zenye bei ya chini sana ya huduma za umeme  ,

"Ubora wa huduma ya umeme umeimarika sana, kule kukatikakatika saana na mgao wa umeme kumepungua kwa kiasi kikubwa, ingawa hatusemi kwamba ubora sasa umefikia mahali kwamba hakuna shida..., hapana, lakini angalau ubora wa huduma hiyo upo katika kiwango cha kuridhisha na tunaendelea kuboresha ."amesema Mhandisi Mramba 

Vile vile amesema, kwenye maeneo ya gesi asilia EWURA amesaidia sana na anaendelea kufuatilia kwanza kutoa leseni kwa wale wanaojenga vituo hasa vya gesi iliyokandamizwa (CNG) pamoja na vituo vya mafuta, lakini pia anasimamia kuhakikisha kwamba huduma zinazotolewa na vile vituo vinakidhi mahitaji ya jamii.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mramba,wajibu wa Wizara ya Nishati ni  kuhakikisha kwamba EWURA anafanya kazi yake kulingana na sheria na sera zilizopo, lakini pia tunamwezesha kutekeleza majukumu yake katika mazingira yanayokubalika ndani ya sekta .

"Kwa hiyo tunaendelea kuwatia moyo watanzania kuwa zipo huduma pia za kiushauri ambazo EWURA anazitoa,zipo huduma za kusikiliza malalamiko na kuyafanyia kazi."amesisitiza

Kwa upande wake Mkurugenzi wa EWURA James Andilile amesema ,EWURA imeingia mkataba na TANESCO kwa lengo la kusimamia utendaji kazi wao ili kuboresha utebdaji na upatikanaji wa umeme ambapo kwa sasa Serikali inafanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Nishati ili kuhakikisha sekta hiyo inaimarika.


Share:

Serikali,wadau waombwa kusaidia vifaa kwa watoto wenye ulemavu

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Katumba (2)Mauyeni kilumbe


NA ESTER MACHA,MBEYA

SERIKALI kwa kushirikiana na wadau wameombwa kuchangia upatikanaji wa vifaa ikiwemo baiskeli kwa watoto wenye ulemavu wa viungo na uoni hafifu katika shule msingi mchanganyiko ya  Katumba (2)iliyopo wilayani Rungwe  mkoani Mbeya .

Akizungumza na Habarinews Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Katumba (2)Mauyeni kilumbe amesema kuwa   shule hiyo ina uhaba wa vifaa saidizi kwa watoto wenye ulemavu kutokana na  wengine kutambaa kutokana na ukosefu wa baiskeli.

Kilumbe ameomba wadau  kutoa misaada mbali mbali  na kusema vifaa vilivyopo havitosherezi  mahitaji ya watoto wenye ulemavu  , wengine wanatumia mashine za kuandikia za nukta nundu  , wenye uarubino wanauhitaqji wa mafuta ,kofia  na mahitaji mengine muhimu .

“Kwasasa hivi tuna baiskeli tano tu ambazo nazo hazitosherezi maana hapa tuna watoto wengine  hawawezi kutembea bila baiskeli    na `zilizopo zina uchakavu  kilichopo hivi sasa tuna uhitaji wa baskeli  16 kwa watoto wenye  ulemavu wasiojiweza kabisa,ila mahitaji zaidi ni  baskeli 16, na mashine 24 za kuandikia  za nukta nundu  kwa wenye uoni hafifu , "amesema

 

Aliongeza kuwa "watoto watano wanatumia vibao vya kawaida hizi mashine mpya tunazofatilia tunaambiwa zimepitwa na wakati lakini kwa mpya kabisa za kisasa ni  shilingi mil.1 hivyo tunaomba wadau na jamii kujitokeza kusaidia watoto hawa “amesema Mkuu huyo wa shule .

Aidha aliomba wazazi kuzidisha upendo kwa watoto wao  wenye ulemavu  kwa  kuwaleta shule kwani  shule hiyo haina malipo yoyote na kusema kuwa kitendo cha kumficha mtoto mwenye ulemavu ndeani ni kumnyima haki ya kupata elimu .

Akizungumzia kuhusu wadau ambao wamekuwa wakisaidia shule hiyo Kilumbe amesema Child Support Tanzania kwa jitihada zake za kuhakikisha kuwa kusaidia wanafunzi wenye ulemavu kwa kutoa vifaa saidizi pamoja  na elimu na kuhamasisha wazazi wanaoficha watoto majumbani kuwapeleka shule.

Kwa upande wake Ofisa elimu Msingi  halmashauri ya Busokelo ,Atuvonwe Chaula amesema kuwa kwa halmashauri hiyo wamekuwa wakifanya jitihada za kuwatumia walimu maalum kwenda vijijini kuwatambua watoto walemavu baada ya wazazi kutambua kuwa watoto wao walikuwa wanaachwa.

Damas Mwambeja ni Mwakilishi wa watu wenye ulemavu aliwataka wadau kuendelea kusaidia shule ya Katumba (2)na kusema licha ya serikali kuwa mstari wa mbele kusaidia shule  hiyo basin a wadau na jamii wana wajibu wa kusaidia vifaa mbali mbali .







Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

  • Habari (2)

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.