CWT yabainisha mafanikio yaliyopatikana kwa walimu katika kipindi Cha mwaka mmoja chini ya uongozi wa Rais Samia



Kaimu Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma


Baadhi ya wajumbe wa Kamati Tendaji ya CWT wakimsikiliza Kaimu Rais Dinnah Mathamani wakati Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma


Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Kaimu Rais wa CWT Dinnah Mathamani wakati Akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali jijini Dodoma.



JOYCE KASIKI,DODOMA

CHAMA cha walimu Nchini (CWT) kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyowajali watumishi nchini katika kutatua changamoto zinazowakabili wakiwemo walimu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma,Kaimu Rais wa Chama hicho Dinnah Mathamani amesema,katika kipindi cha mwaka mmoja Rais Samia tayari ametatua changamoto nyingi za watumishi wakiwemo walimu ikiwa ni pamoja na kulipa madai ya walimu,kupandisha madaraja,ajira,ujenzi miundombinu mashuleni na ahadi ya kuongeza mishara mwaka huu.

Mathamani amesema,katika eneo la upandishwaji madaraja katika mwaka wa fedha wa 2021/22 walimu wapatao 127,000 wamepandishwa madaraja huku walimu 52,000 ambao waliathiriwa na uhakiki wa vyeti nao wakiwa kwenye mpango wa kupandishwa madaraja.

Kuhusu suala la ajira Kaimu Rais huyo amesema,katika kipindi cha mwaka mmoja tayari zaidi ya walimu 27,000 kwa awamu pamoja na 12,000 wanaotarajiwa kuajiriwa itaongeza idadi ya walimu mashuleni na hivyo kuwapunguzia walimu bvipindi na kuwawezesha kujiandaa vyema katika kufudisha wanafunzi vizuri.

Mathamani amezungumzia kuhusu ujenzi wa miundombinu ya shule ambapo amesema jumla ya madarasa 15,000 yamejengwa nchi nzima .

Amesema kupitia kujengwa kwa vyumba hivyo vya madarasa ,sasa wanafunzi hawasongamani madarasani na hivyo kuwafanya walimu kuongeza tija katika kufundisha wanafunzi suala ambalo lina maslahi mapana kwa wanafunzi na Taifa kwa ujumla.

“Suala hili limekuwa ni la msingi sana kwa Taifa,isipokuwa ombi letu kwa Serikali ni kuangalia tatizo la vyoo na nyumba za walimu kwani kuna baadhi ya maeneo hjata nyumba za kupanmga hakuna.”amesema Mathamani

Aidha amesema,CWT kinatambua jitihada zinazofanywa na Serikali katika kutatua tatizo la za walimu nchini ambapo jumla y ash.55.57 bilioni zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu 809 na kuomba utekelezaji na usimamiiz thabiti wa jambo hilo ili liweze kutekelezeka kwa wakati na kupunguza changamoto hiyo.

Kuhusu ulipaji wa madai ya walimu kiongozi huyo amesema,wapo baadhi ya walimu waliokuwa na madai sugu lakini Serikali imelipa madai hayo nab ado inaendelea kulipa madai hayo ya walimu .

“Tunaiomba Serikali ,kwa madai ambayo bado yapo yalipwe kwa wakati ili walimu watulie na shughuli ya kufundisha watoto badala ya kutumia muda mwingi kufiuatilia madai yao.” Amesema na kuongeza kuwa

“Pia tumefarijika kwa ahadi ya Rais Samia ya kuongeza mishahara kwa watumishi ambao miongoni mwao ni walimu …,kwa hiyo suala la mishara mipya tunalisubiri kwa hamu maana tunajua lipo katika hatua za utekelezaji.”

Mathamani ametumia nafasi hiyo kuwasihi walimu wote nchini waendelee kuchjapa kazi kwa bidii ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali kwa kufika katika vituo vyao vya kazi kwa wakati na kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa.

Kiongozi huyo pia ametoa pongezi kwa Rais Samia kwa kuagiza watumishi wakiwemo walimu walioondolewa kutokana na vyeti feki kulipwa asilimia 5 ya mshahara wao waliyokuwa wakichangia kwenye mifuko huku kikipongeza pia agizo la Rais Samia la kutaka waliokuwa wamebakiza muda mfipi kustaafu kupigiwa mahesabu na kupatiwa stahiki zao bila kujali changamoto zozote zilizojitokeza.

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.