Pro.Mkenda:Rasimu ya maboresho ya Sera ya Elimu na Mitaala kupatikana Disemba mwaka huu

Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda (kushoto) akizungumza na wabunge (hawapo pichani) jijini Dodoma wakati akipokea maoni kuhusu maboresho ya Sera ya Elimu na mabadiliko ya mitaala .Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii Stanslaus Nyongo  na wa mwisho ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Eliamani Sedoyeka .

 

                 JOYCE KASIKI,DODOMA

WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema ,atahakikisha  hadi kufikia Disemba mwaka huu  rasimu ya maboresho ya sera ya Elimu na mitaala yake imepatikana .

 Profesa Mkenda ameyasema hayo wakati akifunga mkutano wa kupokea maoni ya wabunge kuhusu maboresho ya Elimu nchini huku akisema kitakachokuwa kimebakia ni kupata idhini ya Serikali ambayo mchakato wa kuipata utaanza Januari 2023. 

Kwa mujibu wa Waziri huyo ,Tanzania inakwenda kuwa na mageuzi makubwa katika sekta ya Elimu ambayo yanaenda kuweka historia nchini ambayo yatakuwa na maslahi mapana kwa Taifa 

"Nawahakikishia  mageuzi ambayo tunakwenda nayo yatakuwa makubwa katika historia ya nchi yetu hatutaki kubahatisha Wala kukurupuka ndio maana tunahitaji sana kusikiliza maoni yenu wabunge,” amesema Prof. Mkenda 

Amesema Dunia ina msukumo mkubwa wa mageuzi ya elimu ndio maana Shirika la Fedha Duniani (IMF) linataka kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa nchi zinazofanya mageuzi kwenye elimu.

Wakitoa maoni yao katika uboreshaji wa Elimu nchini baadhi ya wabunge walishauri kingereza ndio kiwe lugha ya kufundishia huku wengine wakitaka kiswahili kiwe lugha ya kufundishia. 

Aidha wabunge waliotaka kingereza kiwe lugha ya kufundishia wamesema kukataa kingereza kuwa lugha ya kufundishia ni sawa na kumkimbia tatizo badala ya kulitafutia ufumbuzi.

Wamesema,kinachopaswa kufanyika ni kuwanoa walimu  ili wapatikane walimu wenye kuifahamu lugha ya kingereza kiufasaha ambao watawafundisha wanafunzi 

Akichangia maoni katika mkutano huo, Mbunge wa Moshi Vijijini ,Profesa Patrick Ndakidemi (CCM) amesema Tanzania isipotumia kiingereza watanzania watapata tabu kupata ajira nje ya nchi. 

“Kuhusu lugha ya kutumia nitakuwa mkweli, mfano tukisema tunakwenda na kiswahili moja kwa moja ilihali hatutajiandaa kuwa na maneno kamilifu ya kiswahili kwenye sayansi, ukitoka hapa na kiswahili chako ukienda Kenya, Uganda au pengine utabaki hapohapo Tanzania.

“Mawazo yangu kuhusu lugha ni kwamba lugha ya kiingereza inatumika duniani kote, hivyo tuipe kipaumbele la sivyo tutakapotoka hapa kwenda kwa wenzetu tutapigwa goli,” alisema. 

Amesema kuwa Wakenya wanawazidi Watanzania katika sokon la ajira kwa sababu wanajua kiingereza.

“Wakienda huko kwingine wanapewa kipaumbele, kwa hiyo tuhimize kiingereza kitumike na Kiswahili kitumike pale panapostahili,” amesema. 

Kwa upande wake  Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Shari Raymond  amesema yapo baadhi ya masomo kama kemia ,bailojia na masomo mengine ni ngumu kufundishia kwa kiswahili.

"Kwa hiyo hapa naona kingereza kibaki kuwa lugha ya kufundishia,maana bado hatujafikia wakati wa sisi kutumia lugha yetu Kiswahili kufundishia masomo, kiingereza kipewe kipaumbele tena kianze  kutumika kuanzia darasa la kwanza,”  amesema Shari  

Aidha, Mbunge wa Singida Kaskazini, Ramadhan Ighondo (CCM) amesema lengo la kumpeleka mtoto shule ni kuboresha maarifa na siyo lugha.

“Utafiti niliofanya ni kwamba watoto wetu wanapotoka shule ya msingi wanatoka wakiwa na uelewa lakini wakifika sekondari wanakunja sura..,tatizo siyo watoto wakajue lugha, tunataka wakapate maarifa, wakienda China wanajifunza kwanza kichina ndipo wajifunze udaktari, Urusi na Japan vilevile, tuondoe boriti kwamba kiswahili ni lugha masikini tuweke watalaam, watafsiri misamiati ya kisayansi,” amesema. 

 Mbunge wa Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo kwa upande wake ametolea mifano nchi za Asia kama vile Singapore kuwa inatumia kiingereza na kufanikiwa kukua kiuchumi.

"Badala ya kulikimbia tatizo ni vema kulitibu kwa maana kuwa kama hakuna walimu wa kingereza, wafundishwe na kupatikana walimu stahiki wa kufundisha lugha hiyo.

Pia ameiasa Serikali  iondoe kodi kwa wamiliki wa shule binafsi ili wajitokeze wengi kufungua shule nyingi na kupunguza uhaba wa ajira za walimu nchini.

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.