|
Waziri
wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akiwasilisha Bungeni
jijini Dodoma maombi ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa
2022/23. |
JOYCE KASIKI,DODOMA
WIZARA ya Uwekezaji
,Viwanda na Biashara imeomba kutengewa
kiasi cha sh.99.105 bilioni katika Mwaka wa fedha wa 2022/2023 huku ikitaja
vipaumbele vyake katika kipindi hicho.
Akisoma hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi
katika mwaka wa fedha wa 2022/23,Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Ashatu Kijaji
ametaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na Miradi ya kipaumbele iliyopo
katika Mipango na Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 inaanza
utekelezaji, kuondoa urasimu katika kuhudumia wawekezaji na wafanyabiashara,kuimarisha
ushiriki wa Sekta Binafsi moja kwa moja katika uchumi na uwezeshaji wa
wananchi.
Aidha amesema vipaumbele mahususi katika kipindi hicho ni pamoja na kuendelea
kuratibu programu za uhamasishaji wa uwekezaji ndani na nje ya nchi,kuratibu
masuala ya uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi,
kuratibu ufanikishaji wa uwekezaji ikiwemo
kuongeza ufanisi wa miradi ya uwekezaji kupitia
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Aidha
Dkt.Kijaji amesema,Serikai imefanya tathimini ya upandaji wa bei za bidhaa
nchini na kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutafuta vyanzo
mbadala vya upatikanaji wa bidhaa hizo ili kukidhi mahitaji.
“Serikali
inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za bidhaa muhimu hususan
zile zilizoonekana kuathiriwa na UVIKO-19 sambamba na vita kati ya Ukraine
na Urusi,kuwaagiza wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa muhimu kushusha
mara moja bei za bidhaa walizopandisha pasipo kuendana na uhalisia wa bei
ya soko na kuuza bidhaa husika kwa kuzingatia gharama halisi za uingizaji,
uzalishaji na usambazaji.”amesema Dkt.Kijaji
Pia
amesema Serikali inawaelekeza wazalishaji wa bidhaa muhimu kuzalisha na
kusambaza bidhaa husika kulingana na uwezo wa viwanda uliosimikwa,wauzaji
na wasambazaji wa mbolea zenye bei elekezi wahakikishe wanazingatia bei
zilizopangwa na Serikali.
Dkt.
Kijaji amesema Tume ya Ushindani (FCC) imeelekezwa kufuatilia kwa karibu
mwenendo wa biashara wa bidhaa muhimu ambazo katika tathmini iliyofanyika
zimeonesha kuathirika zaidi na upandaji wa bei.
xxxxxx
|
Na
Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI
wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikai
imefanya tathimini ya upandaji wa bei za bidhaa nchini na kuchukua hatua
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutafuta vyanzo mbadala vya upatikanaji wa
bidhaa hizo ili kukidhi mahitaji.
Dkt.
Kijaji ameyasema hayo leo Ijumaa tarehe 6 Mei, 2022 bungeni jijini Dodoma
wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2022/23.
Dkt.
Kijaji amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za
bidhaa muhimu hususan zile zilizoonekana kuathiriwa na UVIKO-19 sambamba na
vita kati ya Ukraine na Urusi.
Ametaja
hatua nyingine ni kuwaagiza wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa muhimu
kushusha mara moja bei za bidhaa walizopandisha pasipo kuendana na uhalisia
wa bei ya soko na kuuza bidhaa husika kwa kuzingatia gharama halisi za
uingizaji, uzalishaji na usambazaji.
Pia
amesema Serikali inawaelekeza wazalishaji wa bidhaa muhimu kuzalisha na
kusambaza bidhaa husika kulingana na uwezo wa viwanda uliosimikwa; wauzaji
na wasambazaji wa mbolea zenye bei elekezi wahakikishe wanazingatia bei
zilizopangwa na Serikali.
“Wale
wote watakaokiuka watachukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwa ni pamoja na
kufutiwa leseni za biashara"Amesema.
Dkt.
Kijaji amesema Tume ya Ushindani (FCC) imeelekezwa kufuatilia kwa karibu
mwenendo wa biashara wa bidhaa muhimu ambazo katika tathmini iliyofanyika
zimeonesha kuathirika zaidi na upandaji wa bei.
“Serikali
imeendelea kushawishi na kuvutia Wawekezaji wa ndani na nje kwenye
uzalishaji wa mazao ambayo tumekuwa tegemezi kwa kiwango kikubwa kutoka nje
ya nchi ikiwa ni pamoja na mafuta ya kula, sukari na ngano.
Amesema
lengo ni kupata uzalishaji unaotosheleza mahitaji ya soko letu la ndani na
hatimaye kuuza nje.
|
Pia kuratibu uanzishaji na uendelezaji wa miradi
mikubwa ya uwekezaji yenye manufaa mapana kwa Taifa,kuimarisha mifumo ya kushughulikia
changamoto za uwekezaji,kuboresha mazingira wezeshi ya kuendeleza viwanda na
biashara kwa kupitia na kutunga sheria,sera na mikakati ya kuvutia
uwekezaji,kuimarisha na kuhamasisha uwekezaji wa Sekta Binafsi katika Maeneo
Maalum ya Kiuchumi (SEZ) na Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa ajili ya
uzalishaji wa bidhaa zitakazouzwa nje (EPZ),kuimarisha taasisi za utafiti na
kufanya tafiti kwa ajili ya maendeleo ya viwanda,kuhamasisha uwekezaji wa
viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana kwa wingi nchini na bidhaa
zinazotumiwa kwa wingi nchini kama vile nguo, mafuta na sukari, kuendeleza
viwanda vya usindikaji vinavyozalisha bidhaa za petroli (Petro-gas),
kemikali, uzalishaji wa dawa za binadamu na vifaa vya ujenzi.
|
|
No comments:
Post a Comment