JOYCE KASIKI,DODOMA
Katika bajeti ya mwaka wa Fedha wa 2022/23 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya kuendeleza wabunifu ili bunifu zao ziweze kuingia sokoni.
Aidha Serikali imesema,tayari imewatambua wabunifu 200 ambao bunifu zao zilizofanya vizuri katika Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) katika miaka iliyopita ambapo jumla sh.bilioni 2.3 zimetumika kwa ajili ya kusapoti bunifu hizo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Eliamani Sedoyeka ameyasema hayo Mei 4,mwaka huu wakati akifungua afunzo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma yaliyolenga kuwajengea uwezo kuhusiana na masuala ya ubunifu ili waweze kuelimisha umma kuhusiana na Maonyesho ya MAKISATU ya mwaka huu yanayoatarajia kuanza Mei 15-Mei 20 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Maonyesho ya MAKISATU mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo’ubunifu kwa Maendeleo enedelevu.
Profesa Sedoyeka amesema Serikali imekuwa ikitenga na kutumia fedha hizo kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya kubuni na kuendeleza bunifu na kuzijengea uwezo taasisi au mbunifu mmoja mmoja ili bunifu zao ziweze kuingia sokoni.
Profesa Sedoyeka amezungumzia kuhusu zawadi za washindi wa MAKISATU 2mwaka huu ni shilingi ilioni tano kwa mshindi wa wa kwanza,milioni tatu kwa mshindi wa pili na shilingi milioni mbili kwa mshindi wa tatu.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo ,kwa wale watakaoingia fainali ya mashindano hayo watapata fursa ya bunifu zao kuendelezwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Maulilio Kipanyula alisema jumla ya wabunifu 862 wanatarajiwa kushiriki katika maonyesho hayo kutoka katika makundi saba.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanahabari waliopata mafunzo hayo ambaye pia ni Balozi wa Mazingira Sakina AbdulMasoud alisema,watayatumia mafunzo hayo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusiana na masuala ya ubunifu.
Aidha amewaasa wanahabari kukumbuka kuelimisha wabunifu kuhusiana na masuala ya utunzaji wa mazingira pindi wanapotengeneza bunifu zao.
No comments:
Post a Comment