Afisa wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango,Utafiti na Tathimini ya Mitihani Dkt.Alfred Mdima akionyesha mfumo wa kutumia kishikwambi katika usahihishaji mitihani na ufundishaji watoto wengi darasani kupita kiasi.

 

              JOYCE KASIKI,DODOMA

BARAZA la Mitihani la Taifa limekuja na suluhisho la kumwezesha mwalimu kumudu darasa lenye wanafunzi wengi kupita kiasi pamoja na mfumo wa usahihishaji mitihani kidigitali.

 Afisa wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango,Utafiti na Tathimini ya Mitihani Dkt.Alfred Mdima amesema,mifumo yote miwili ni ya kidigitali ambayo inatumia kishikwambi.

“Tumekuja hapa katika maonyesho haya ya Kitaifa ya Ubunifu ya Sayansi na Teknolojia ,tumeleta mifumo miwili ,mfumo wa kidigitali wa usahihishaji wa mitihani ambao msahihishaji anapelekewa maswali na kuyasahihisha kidigitali na anarudisha majibu kwa mratibu wa Baraza la Mitihani kidigitali,

“Lakini pia tumebuni mfumo mwingine wa kutatua tatizo la ufundishaji na upimaji wa wanafunzi darasani walio wengi kupita kiasi,ufumbuzi wa suala hili sasa umepatikana “amesema Dkt.Mdima

 Kwa mujibu wa Dkt.Mdima , hata wanafunzi wakiwa wengi kiasi gani ,kwa kutumia mfumo wa ufundishaji kidigitali,mwanafunzi anaweza kujifunza kwa ufanisi na wakapata umahiri unaotakiwa kulingana na mtaala waliowekewa na Taasisi ya Elimu Tanzania .

“Sisi Baraza la Mitihani kwa ufadhili wa shirika la watoto Duniani (UNICEF),tumeweza kuja na mfumo ambao ni suluhisho la tatizo la ufundishaji na upimaji katika madarasa yenye watoto wengi kupita kiasi ,yaani sasa hivi watoto wengi darasani kupita kiasi siyo tatizo tena kwa sababu tumekuja na suluhisho lake ambalo ni kwamba ,mfumo huu kwa kutumia vishikwambi tumechukua mada zote kuu na mada mahususi tumeziweka ndani ya hiki kishikwambi,

“Tumetengeneza maswali mengi ya kutosha kwa kila mada mahususi na aina nyingi ili yaweze kumsaidia mwanafunzi kujifunza zaidi..,Mfumo huu una shughuli nyingi za kutendwa na mwanafunzi na wanafunzi wanapenda sana vishikwambi hivyo kutokana na mfumo ulivyosetiwa utamwezesha mwanafunzi kujifunza kwa umahiri zaidi.” 

Amesema,wakati mwanafunzi akijibu maswali kwa kutumia kishikwambi ,kunakuwa  na kishikwambi kingine ambacho kimeunganishwa na mwalimu ambapo kinamuonyesha mwalimu kwamba mwanafunzi amepata ama amekosa na anapofika mwisho kishikwambi kinamwambia mwanafunzi amepata alama ngapi kati ya tano ambapo kama amepata zote kishikwambi kinampa motisha ya kikatuni ambacho kinammotisha na kumfanya mtoto anakuwa na umakini wa ujifunza muda wote.

Pia amesema kishikwambi hicho kinamsaidia sana mwalimu kwa sababu mwalimu sasa hatakuwa na lundo la madaftari ya kusahihisha kwani kazi zote watoto wamefanya kwenye vishikwambi na rekodi zote zinahifadhiwa kwenye kishikwambi hicho ambapo kazi ya mwalimu ni kuangalia tu kwamba mtoto amepata alama ngapi kwani anakuwa amewasajili wote kwenye kishikwambi kwa picha na jila la mtoto.

“Hapa hata kama mwalimu angekuwa na wanafunzi 1000 darasa ili mradi kila mtoto ana kishikwambi chake ,bado mwalimu atafundisha kwa urahisi sana katika darasa lake..,”amesisitiza 

Dkt.Mdima amesema kishikwambi hicho kimewekwa kazi za masomo tu na mwanafunzi hana namna yoyote ya kufanya jambo lingine lisilohusiana na masomo lakini pia hakitumii mtandao wa internet badala yake mwalimu na mwanafunzi watawasiliana kupitia njia ya bloototh.

“Tunaamini kwa serikali yetu ilivyo sikivu haiwezi kushindwa kumpatia mwanafunzi kishikwambi ,ni suala la maamuzi na kupenda elimu kila mwanafunzi wa Tanzania atakuwa na kishikwambi,

“Tatizo hili la wananfunzi wengi madarasani limechukua muda mrefu sana sisi tumekuja na suluhisho tunaomba serikali ituunge mkono

Kishikwambi kimewekwa programu za masomo tu ,hiki ni kwa ajili ya kujifunza na kufundisha tu,kwa hiyo hakina mambo mengine zaidi ya kujifunza na hawezi kudaownload kitu chochote.”amesema

Ametaja faida nyingine za mfumo huo kuwa ni kumwezesha mwanafunzi kuwa mahiri na kuwa na kasi ya kutenda na usahihi unaotakiwa katika kutenda ambao unapatikana baada ya mwanafunzi kufanya mazoezi mengi iwezekanavyo .

 “Wanafunzi wameweza kufanya kazi kwa kasi inayotakiwa kasi na usahihi unaotakiwa kwa sababu mwanafunzi anapokuwa anafanya maswali hayo katika kishikwambi ukifika ule muda wa dakika moja kama hajamaliza maswali yanaondoka zitakaporudia tena mtoto akili itakuwa imeshamkaa sawa kwamba nikifanya kwa uzembe maswali yataondoka na nitapata sifuri kwa hiyo baada ya muda kishikwambi kinamzoeza mwanafunzi kuwa ni mtu wa kasi .”

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.