JOYCE KASIKI,DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amewataka watumishi wa umma kuendela kufanya kazi kwa kuzingatia maadili,sheria,miongozo na taratibu za Utumishi wa Umma katika kuwahudumia wananchi.
Akifunga kikao kazi cha wakuu wa Idara na vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimawatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma,Waziri Bashungwa amesema,uzingatiaji wa sheria ,miongozo na taratibu za Utumishi wa Umma kunaongeza tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Vile vile Bashungwa amewataka wakuu wa hao wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kutekeleza wajibu wao bila kuwaonea watumishi walio chini yao.
Aidha amesema kwa upande wa Serikali itaendelea kusimamia Watumishi wa Umma kwa ujumla ili wafanye kwa kuzingatia nidhamu na uwajibikaji katika Utumishi wa Umma katika kuwahudumia wananchi.
Awali ,Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi amewataka wakuu hao wa Idara na Vitengo vya vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimawatu katika Utumishi wa Umma kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma kwa haraka.
No comments:
Post a Comment