JOYCE KASIKI,DODOMA
MBUNGE wa Bahi Kenneth Nollo (CCM) amehoji mpango wa Serikali wa kujenga daraja la kudumu kwenye mto Mzizima ili barabara ya Kigwe hadi Chipanga iweze kupitika katika majira yote ya mwaka.
Nollo ametoa kauli hiyo
leo wakati akiuliza swali la msingi Bungeni jijini Dodoma huku akisema ujenzi wa daraja hilo utasaidia kuondoa kero ya wananchi kutumia
muda mwingi wa kusubiria maji ya mto yapungue pindi inaponyesha mvua ili wavuke na kuendelea na
shughuli za kiuchumi na kijamii.
“Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga daraja la kudumu kwenye mto Mzizima ili barabara ya Kigwe hadi Chipanga Wilayani Bahi iweze kupitika mwaka mzima?”amehoji Nollo
Akijibu swali hilo Naibu Waziri
Ofisi ya Rais ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David
Silinde alisema,katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia TARURA Wilaya ya
Bahi, imetenga fedha kiasi cha Shilingi milioni 620.23 kwa ajili ya ujenzi wa
Daraja (Box culvert) lenye urefu wa mita 34.
“Ujenzi wa daraja hili umeanza
Februari 20
, 2022 na unatarajiwa kukamilika Agosti 19, 2022 na ujenzi wa mradi huu
umefikia asilimia 30,kazi hiyo inafanywa
na Mkandarasi RAVJI CONSTRUCTION LTD.”amesema Silinde
Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo,kukamilika
kwa ujenzi wa daraja hilo utaifanya barabara ya Kigwe – Chipanga kupitika wakati wote na hivyo kuondoa kero ya wananchi kutumia
muda mwingi wa kusubiria maji ya mto yapungue ili wavuke na kuendelea na
shughuli za kiuchumi na kijamii.
No comments:
Post a Comment