Zingatia haya wakati kuomba maombi ya kazi za muda katika sensa ya watu na Makazi 2022






               

 






  JOYCE KASIKI,DODOMA


 

MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Dkt.Albina Chuwa amewataka waombaji wa nafasi za kazi za ukarani na usimamizi wa Sensa inayotarajiwa kufanyika hapa nchini Agosti 23 mwaka huu,kujaza fomu za maombi kwa uhakika ili kujiweka kwenye nafasi ya kupata ajira hizo za muda.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma,Dkt.Chuwa amesema maombi mengi yaliyotumwa yameonekana kuwa na  changamoto ambazo amezitaja kuwa ni pamoja na kutojaza taarifa sahihi kama vile barua pepe na namba za simu na hivyo kushindwa kupokea neno la siri na taarifa nyingine muhimu za kumwezesha mwombaji kuendelea kukamilisha maombi yake.

 

“Mwenendo wa uombaji tangu kutangazwa kwa nafasi hizi tangu Mei 5 mwaka huu unaendelea vizuri nchi nzima ,hdi kufikia saa saba kamili leo mchana (Mei 10,2022),waombaji wapatao 119,468 walikuwa tayari wameshatuma maombi yao kupitia mfumo wa kielektroniki kati ya nafasi 205,000 zinazohitajika.”amesema Dkt.Chuwa

 

 Vile vile amesema,waombaji kusahau  jina la mtumiaji na neno la siri hivyo kushindwa kuhuisha na kutuma fomu namba 1 iliyoidhinishwa na mwajiri kwa waajiriwa na viongozi wa serikali za mitaa.

 

“Ni kitu cha ajabu,umeshaprint fomu,unapeleka kwa mwajiri ili akujazie au kwa serikali ya mtaa akujazie ili uje uiweke kwenye mtandao kwa mara ya pili mtu unasahau ile namba uliyotumia ,unasahau ile email address uliyotumia ,hii nayo ni changamoto ambayo tumeiona na tukaona tueleze wananchi kupitia vyombo vya habari .”amesema Dkt.Chuwa

 

Dkt Chuwa ametaja changamto nyingine kuwa ni waombaji kutokuwa na baadhi ya taarifa kama vile namba yakitambulisho cha Taifa (NIDA) ,waombaji kutokuwa na nyaraka za lazima za kuamatanisha kama vile cheti cha kuzaliwa na waombaji kuwa katika maeneo yenye mtandao hafifu hivyo kupata changamoto ya kutuma na kuuhisha maombi.

 

“Hapa kinaweza kutumika kitambulisho cha kura,kitambulisho cha Mkaazi kwa upande Zanzibar hata leseni ya udereva.”amesema na kuongeza kuwa

 

“Waombaji wote wenye nia ya kuomba tuwe makini kuhakikisha viambatanisho vyote tunavyo nan i sahihihi,tuwe makini kusoma muongozo wa maombi ya kazi,tuwe makini na namba zetu za simu tunazozitumia kupoea taarifa zetu pamoja na Email address,tutunze namba zetu za siri tunazozitumia

Kazi tunayoenda kuifanya ni itanedeshwa kidigitali kwa hiyo tunakiwa kuwa makini kwani tunakwenda kufanya sense ambayo inakwenda kutuletea takwimu sahihi zaidi.”amesema na kuongeza kuwa

 

Wakati wa kuingia kwenye mfumo na usome ipasavyo kabla hujajaza Fomu Na.1 na hakikisha unafuata maelekezo yote ikiwemo kujaza taarifa zako kwa usahihi ili kuondoa usumbufu wa kuhuisha taarifa mara kwa mara.”amesisitiza Dkt.Chuwa

 

Pia amewataka kujaza namba ya simu na barua pepe ambayo inatumika kwa sasa ili mwombaji aweze kupokea taarifa za akaunti yake kuingia kwenye mfumo ili kukamilisha kutuma maombi ya kazi.

 

Kwa mujibu wa Dkt.Chuwa unapochapisha Fomu Na.1 ya maombi ya kazi ya sensa hakikisha unaisanisha kwa wahusika na kuirejesha kwenye mfumo mapema ili kuamilisha kutuma maombi ya kazi .

 

Pia amesema,jambo lingine ni kuandaa viambatisho muhimu kama vile cheti cha kuzaliwa ,cheti cha kidato cha nne na picha,namba ya kitambulisho cha NIDA ili wakati wa kujaza fomu usikwame na hakikisha unapitia maswali yote yanayoulizwa mara kwa mara ili kukurahisishia kupata majibu ya haraka maswali ambayo yalishaulizwa.

 

Aidha amesema,kwa wale watanzania ambao hawana vyeti vya kuzaliwa ,kiapo cha mahakamani kinaweza kutumika kama mbadala wa veti hivyo .

 

“Kumbuka Fomu NA.1 ya maombi ya kazi ya sense inapatikana bila malipo na inajazwa kupitia mfumo wa maombi ya kazi za sense bila malipo na mwisho wa kupokea maombi hayo ni Mei 19 mwaka huu saa sita kamili usiku.”

 

 


Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.