Angalia namna Serikali inavyokwenda kubotesha sekta ya Elimu nchin




JOYCE KASIKI,DODOMA

WIZARA ya Elimu Sayansi na Teknolojia imeomba kuidhinishiwa na Bunge kiasi cha Trilioni 1.493 ili kuiwezesha kutekeleza shughuli za wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/23 huku ikisema pamoja na mambo mengine,inakwenda kufanya mabadiliko makubwa katika sekta ya Elimu nchini.

Akisoma hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2022/23 Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema,kazi kubwa itakayofanyika katika Mwaka wa Fedha wa 2022/23 ni kufanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 kwa minajili ya kufanya maamuzi kuhusu baadhi ya mambo ambayo Sera imeyaainisha lakini hayajatekelezwa.

"Kwa mfano, Sera inaainisha kwamba elimu ya lazima, yaani ‘compulsory education’, itakuwa ni ya miaka kumi, lakini bado tunatoa elimu ya lazima ya miaka saba.”amesema na kuongeza kuwa

"Tunatarajia kuwa kabla ya mwisho wa mwaka huu uchambuzi utakuwa umefanyika na kukamilika kuhusu Sera hii ili maamuzi yaweze kufanyika kuhusu utekelezaji.”

Kwa mujibu wa Waziri huyo ,pamoja na uchambuzi huo, juhudi zitaendelea za kukusanya maoni ya wadau wote ili maamuzi yatakapofanyika yazingatie maoni ya wadau wote na uchambuzi wa kitaalam.

Aidha amesema ,mapitio ya Sera yatatoa dira ya mabadiliko yatakayohitajika katika Sheria ya Elimu ya Mwaka 1978 huku akisema matarajio ni kuwa ifikapo Desemba 2022 Wizara itakuwa imekamilisha rasimu ya mabadiliko ya mitaala itakayozingatia maoni ya wadau na mwelekeo wa Sera ya Elimu utakaokuwa umependekezwa.

" Zoezi hilo litazingatia sana uboreshaji wa elimu na utaongeza sana elimu ya ufundi na ujuzi itakayomsaidia mhitimu kuweza kujiajiri na kuajirika.

Profesa Mkenda amesema,mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo na mabadiliko ya mitaala ambayo Serikali inakusudia kukamilisha yataleta mageuzi makubwa ya elimu ambayo hayajawahi kutokea hapa nchini.

Waziri Mkenda ametoa wito kwa wadau kuendelea kutoa maoni yao kwa sababu azma ya Serikali ni kufanya mageuzi makubwa yanayozingatia matakwa ya wananchi, kuongeza ubora wa elimu, kuwezesha wahitimu kujiamini, kuajirika na kujiajiri na pia kuwawezesha wahitimu kumudu utandawazi na kukidhi mahitaji ya uchumi wa nchi yetu.

Amesema katika mwaka huo wa fedha wizara hiyo pamoja na mambo mengine itazingatia nakuangalia zaidi katika Mapitio ya Sera,Mapitio ya Sheria,Mabadiliko ya Mitaala, Idadi (mahitaji) ya Walimu, Wakufunzi na Wahadhiri, Ubora Stahiki wa Walimu, Wakufunzi na Wahadhiri,mahitaji ya Miundombinu na Mahitaji ya Vitendeakazi.

"Masuala haya saba ni budi yazingatiwe ili kuhakikisha kwamba mageuzi ya elimu tunayoyatarajia yatakuwa kweli yanakidhiMahitaji yetu. “amesisitiza Profesa Mkenda


Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.