Wanafunzi wa kike wahimizwa kusoma badala ya kujihusisha na vitendo vya ngono







ESTER MACHA,MBEYA


NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maruprisca Mahundi amewaasa wanafunzi wa kike kusoma kwa bidii badala ya kuendekeza vitendo vya ngono zisizo salama kwa kutumia Kinga ya kurejeshwa shuleni hata kama watapata ujauzito.
Amesema uamuzi huo wa serikali wa kuwarejesha shuleni wanafunzi wa kike wanaoachanshule kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata ujauzito ni kuhakikisha kundi Hilo linasoma na kufikia malengo yao na siyo vinginevyo.

Mhandisi Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya wakati wa uzinduzi wa wimbo wa kuelimisha wanafunzi na jamii kujikinga na magonjwa ya zinaa kupitia Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na kuhusishwa wanafunzi zaidi ya 60 wa Shule ya Sekondari ya Wasichana na Loleza Jijini Mbeya.

Amesema uamuzi huo wa Serikali utumike vizuri kwani imeamua kuwekeza kwa watoto wa kike wanaopata mimba kurudi shuleni baada ya kujifungua ili wasome kwa bidii zaidi.

Mhandisi Mahundi amesema kuwa wanafunzi wanatakiwa kutoitumia vibaya elimu wanayoipata kwani wazazi na Serikali wamewekeza kwao ili kuja kuishi maisha mazuri na kazi nzuri sasa kitendo cha kushindwa kusoma kwa budii na kudanganyika na bodaboda kinawapotezea muda lakini pia wanajiweka katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa.

''Taarifa ya Shule imenisikitisha sana kwa shule yenye vipaji kama hii vya wanafunzi na kutoa wanafunzi bora kuwepo kwa baadhi yenu kuacha masomo kutokana na kupata ujauzito jambo ambalo halipendezi''amesema Naibu waziri .

Kwa upande wake Mtafiti kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) mkoani Mbeya Dkt.Ruby Mcharo amesema wastani wa asilimia 21 ya wanafunzi 504 wa Vyuo Vikuu nchini waliopimwa wamebainika kuwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa huku wanawake wakiwa ni asilimia 21 huku wanaume wakiwa ni asilimia 14 kwa takwimu za mwaka 2019/2021.

Aidha Dkt.Ruby amesema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya makundi ya vijana wenye umri kati ya miaka 18 mpaka 21 kukutwa na magonjwa zinaa licha ya kuwepo kwa kampeni za utoaji elimu ya mara kwa mara ili kunusuru kundi hilo inayotolewa na watafiti kutoka NIMR kwa kushirikiana na wataalam wa afya.

''Tafiti za maambukizi kwa wanavyuo ni kubwa na Changamoto kubwa ni kufanya ngono zisizo salama na wameona sasa kuwafikishia elimu kwa njia za wimbo kwa makundi mbalimbali ''amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ,Dkt. Rashid Chuachua , amesema Shule ya Sekondari ya Wasichana Loleza imekuwa ikifanya vizuri sana katika masuala ya afya hivyo ni wakati sasa kwa Taasisi hiyo kuongeza weredi kwa kutoa elimu bora ya kujikinga na magonjwa ya zinaa.

Mwanafunzi wa kidato cha Sita ambaye yupo kwenye mradi huo ,Catherine Mwajebele ameomuomba Naibu Waziri kuendelea kuwakumbuka na kuwashika mkono kupitia Taasisi yake ya Maryprisca Women Empowerment fund.

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.