Wiki ya Ubunifu yapamba moto Dodoma

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma (hawapo pichani) kuhusu wiki ya Mashindano ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yanayoanza mkoani Dodoma Mei 15-Mei 20 mwaka huu.

 

                 JOYCE KASIKI,DODOMA

 

RAIS wa Zanzibar Dkt.Hussein Ally Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya Kitaifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu yatakayoanza Mei 15 hadi Mei 20 mwaka huu mkoani Dodoma.

Aidha Maonyesho hayo yatafunguliwa rasmi Mei 16 mwaka huu huku yakitarajiwa kuhitimishwa mnamo Mei 20 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu wiki ya ubunifu,Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema, katika maonyesho ya wiki ya ubunifu , pamoja na mambo  mengine yataambana na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) na semina itakayolenga kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wabunifu.

Amesema maonyesho hayo yanatoa fursa kwa wabunifu na wagunduzi kuonyesha Kazi zao kwa wadau na wanunuzi wa bidhaa wanazozitengeneza.

Aidha Profesa Mkenda amesema licha ya Mashindano hayo kufanyika kitaifa mkoani  Dodoma lakini maadhimisho hayo yamefanyika kwa ngazi ya mikoa tangu April 27 Mwaka huu na yanatarajiwa kuhitimishwa Mei 14 mwaka huu.

 

XXXXXXX








Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.