Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge Sera na Uratibu George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma(hawapo pichani).
JOYCE KASIKI,DODOMA
SERIKALI imesema mchakato wa kuwapata makarani na wasimamizi wa Sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu ,umeanza leo Mei 5 hadi Mei 19 mwaka huu ambapo waombaji ni wenye umri Kati ya miaka 18 hadi 45.
Aidha Serikali imewaonya watu wenye nia isiyo njema kwa zoezi la sensa ambao wamekuwa wakijaribu kutoa matangazo ya ajira za Sensa kwa nia ya kluwatapeli wananchi wanaohitaji kushiriki katika zoezi la Sensa huku ikielezwa kuwa kwa wote watakaobainika watasakwa na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge Sera,uratibu ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu George Simbawene ameyasema hayo leo Mei 5,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ajira hizo za muda katika maandalizi ya kuelekea kwenye Sensa.
Amesema,ajira hizo zitaombwa kupitia mtandao na hazitahusisha malipo ya aina yoyote kwa mwombaji wa ajira huku akisema mchakato wa kuchambua maombi ya kazi pamoja na usaili utasimamiwa na Kamati Maalum itakayoundwa katika ngazi ya kila wilaya.
Aidha amesema usaili utafanyika katika ngazi ya wilaya kwa wasimamizi wa TEHAMA
“Niwaombe watanzania wote wenye sifa ambao wangependa kuomba nafasi za ajira za makarani na wasimamizi wa sensa kufuata utaratibu uliowekwa kwa ukamilifu ili kuomba nafasi hizo ambazo kazi za kufanya pamoja na sifa za mwombaji zimebainishwa katika tangazo la ajira za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022.”amesema Simbachawene na kuongeza kuwa
“Mfumo wa kuomba ajira hizi kupitia mtandao unapatikana kupitia www.pmo.go.tz,www.tamisemi.go.tz,www.nbs.go.tz kwa Tanzania Bara na www.ompr.go.tz,https//www.tamisemim.go.tz au www.ocgs.go.tz kwa wale wanaoomba Tanzania Zanzibar na kupitia tovuti hizo waombaji watapata tangazo kamili la kazi lenye orodha ya nafasi zilizopo katika sense pamoja na vigezo vinavyohitajika.”
No comments:
Post a Comment