Mhagama awafunda wakuu wa Idara katika Utumishi wa Umma

Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

 

 

 

JOYCE KASIKI,DODOMA

WAZIRI wa Nchi ,Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama amewataka wakuu wa Idara na vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasimaliwatu katika Utumishi wa Umma kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo huku wakienda na kasi ya utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo ya nchi.

Akizungumza katika kikao kazi cha watumishi hao jijini Dodoma  ,Waziri Mhagama amesema, wakuu hao wa Idara wana kila sabahu ya kuona uzito wa kikao hicho na yatakayoazimiwa kwa kwenda kuyafanyia kazi kikamilifu kwa lengo la kwenda na kasi ya utendaji kazi ya Rais Samia ili kufikia malengo ya Taifa katika kufikia maendeleo endelevu.

“Kuna kila sababu ya kufanya mabadiliko ya haraka na kwenda kasi ya Rais Samia ambaye ameshajipambanua na kufanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.”alisema Mahagama na kuongeza kuwa

“Rais Samia anaongozwa na shabaha ,malengo na ubunifu katika kuhakikisha kunakuwa na utekelezaji wa mikakati mingi ya kujenga ustawi wa nchi yetu.”

“Lazima tuenende katika maazimio na utendaji kazi wa Rais Samia hakika tutapata maendeleo ya haraka sana.

Aidha amewataka wakuu hao wa Idara kufuata sheria na kanuni zinazowaongoza katika utendaji kazi hasa katika kushughulikia tuhuma za watumishi wanapokuwa na makosa.

Amesema watumishi wa umma wamekuwa na malalamiko yanayochukua muda mrefu bila kushughulikiwa hali ambayo inaigharimu Serikali kutokana na mtumishi husika kuendelea kulipwa stahiki zake.

                                                                     

“Wakati mwingine watumishi hukosa haki zao bila sababu ,unakuta anazunguka na faili la nidhamu kwa muda mrefu bila kushughulikiwa,

“Malalamiko ni mengi ,mashauri hayafungwi kwa wakati maana mtumishi anapokuwa anatuhuma bado anastahili kulipwa,changamoto ni kwamba mashauri haya hayafungwi kwa wakati hii ni hasdara kwa serikali.”amesema Mhagama

Vile vile amesema,watumishi wamekuwa wakilalamika kuhujumiwa na maafisa rasilamiwatu huku akiwaonya mara moja kuacha kuwahujumu watumishi na badala yake wafanye kazi zao kwa kuzingatia sheria kanuni na miongozo inayowangoza katika kushughulikia changamoto za watumishi wa umma.

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.