MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Dodoma Ahidi Sinene akipanda akiongoza zoezi la upandaji miti katika eneo la Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe jijini Dodoma.   

 
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitalia ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe akimwagilia mti baada ya kuupanda.

Vijana wa JKT wakiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dodoma Ahidi Sinene ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli ya upandaji miti katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Ahid Sinene   


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Ahidi Sinene amewaasa wananchi kwaendelee  kupanda miti kwa wingi kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwemo ya uzinduzi wa Filam ya Royal Tour iliyofanywa na Rais Samia kwa lengo la kutangaza sekta ya utalii nchini.

Akizungumza wakati wa upandaji miti katika hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe,Sinene amesema wanyama hawawezi kuishi mahali ambapo hakuna miti na kwamba ni lazima jamii nchini kote lazima ipande miti ya kutosha.

“Kwenye Royal Tour mle ndani kuna miti ,wanyama wanapenda miti ,kwenye miti kuna dawa lakini pia kuna maua ambayo hayapo mahali pengine popote isipokuwa Tanzania.”amesema na kuongeza kuwa

“Kwa hiyo Rais ameleta utalii mkubwa sana ambao sasa sisi wananchi tunapaswa kuwa wazalendo katika kuunga mkono jitihada hizi za Rais kwa kupanda miti ya kutosha kila mmoja katika mazingira yake na Taasisi kwa ujumla.”

Aidha ameiasa Taasisi ya Mirembe kuhakikisha inaitunza miti hiyo na kukua na kuleta maana sahihi ya kutimiza kampeni ya Rais Samia ya kuikijanisha Dodoma na Taifa kwa ujumla.

“Utunzaji wa mazingira ni madhabahu kama madhabahu nyingine,hata Mungu alianza kuumba mazingira kwanza ndio akamuumba binadamu,kwa hiyo usidharau mazingira ,ukidaharau mazingira umemdharau Mungu wako.”alisisitiza Sinene

Aidha amesema,kampeni ya utunzaji mazingira ilianzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwa Makamu wa Rais huku akisema,sasa ndiye amekuwa Rais mwenyewe kwa hiyo  upele umepata mkunaji .

“Kwa hiyo tunapofanya zoezi hili la upandaji miti ni kutimiza maono  lakini pia ni kumuheshimisha Rais Samia Suluhu Hassan.”amesema

Kwa upande wake Katibu wa Taasisi ya Habari Development Associasion inayojishughulisha na upandaji Miti hapa nchini na  ndio waendeshaji wa shughuli hiyo Bernard James amesema, kwa sasa wamejikikata katika mji Mkuu wa Tanzania Dodoma ili kuukijanisha mkoa huo kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira uliokuwa umefanywa kwa sababu mbalimbali.

Amesema,upandaji huo wa miti ni katika kuitikia maagizo ua Rais Samia ya kutunza mazingira huku akisema katika hospitali hiyo wamepanda miti 2000 ikiwemo miti ya matunda kwa udhamini wa Bakhresa Group.

Bernard amesema,ni imani yake miti hiyo itatunzwa kwa kumwagiliwa vizuri na hatimaye kukua na kutimiza lengo lililokusudiwa la kulifanya eneo hilo kuwa la kijani ,kuvutia , kupata vivuli na matunda .

Katibu huyo ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau walioshiriki na kufanikisha zoezi hilo wakiwemo vijana wa JKT .

“Shukrani kwa Mkuu wa JKT kuruhusu vijana wake kushiriki na kuwezesha upandaji wa miti katika eneo hili la Mirembe.”

Naye Mkurugenzi wa Sheria na Utawala kutoka Bakhresa Group ambao ndio wadhamini wa shughuli hiyo Shani Mligo amesema harakati hizo za upandaji zina manufaa makubwa sasa na vizazi vijavyo.

 “Kwa kuwa Serikali peke yake haiwezi kufanya kazi hii basi tunahamasisha taasisi mbalimbali ,taasisi binafsi kama walivyofanya wenzetu wa habari Development Associasion ,basi na taasisi nyingine ziige mfano huo lakini na wadhamini wengine waige mfano wa Bakhresa Group wa kusapoti zoezi la upandaji miti katika maeneo mengine kwa maslahi ya Taifa letu.”amesema Shani

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Mirembe ambaye pia ni Mtaalam Bingwa wa Saikolojia na Akili  Dkt.Japhet Swai alisema,zoezi hilo limefika Mirembe katika wakati muafaka ambapo kulikuwa na uhitaji mkubwa wa miti.

“Naomba niahidi kwa niaba ya uongozi wa Mirembe kwamba tutajitahidi kadri tutakavyoweza miti hii tuitunze kwa kuimwagia maji hata kufanya ‘replacement’ kama itatokea changamoto yoyote ya kimazingira ambayo itasababisha baadhi ya miti kufa,hii ni katika kuhakikisha miti hii inakua.”Alisema Dkt.Swai

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mazingira wa Jijiji la Dodoma Dickson Kimaro amesema,huo ni mwendelezo wa kukijanisha Dodoma ambayo ilianza kipindi cha msimu wa mvua huku akiwashukuru taasisi ya habari kwa kuendeleza zoezi hilo la upandaji miti.

Ametoa wito kwa wananchi wa Dodoma waendelee kupanda miti hususan ya matunda ambayo licha ya kuleta kivuli lakini pia inakuwa na manufaa katika kuboresha lishe za wananchi

Naye Mdau wa Mazingira Julian Bruno amesema inaleta maumivu anapoona miti inakatwa au inayokufa baada ya kupandwa huku akisema atajitolea kufuatilia ukuaji wa miti hiyo.

“Nimejitolea kufuatilia kuona miti tunayoipanda kama inakufa au inakua ,nimepita maeneo mengi nimeona miti inayokufa siyo mingi ,sasa tumepana miti hapa mimi nitajitolea kupita kila baada ya siku tatu au nne katika eneno hili kufuatilia kuona kama hii miti inastawi.”amesema Bruno

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.