
DODOMA
MBUNGE wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda ameiomba Serikali kupeleka maji Mji wa Tukuyu Kutoka Ziwa Nyasa Ili kusaidia wananchi wa wilaya hiyo kupata maji safi na salama.
Akiuliza swali la nyongeza Bungeni jijini Dodoma Mwakagenda amesema Mji wa Tukuyu hauna maji huku alihoji lini Serikali itapeleka fedha ili kujenga mradi wa kutoa maji Ziwa Nyasa na kuyafikisha Mji wa Tukuyu.
"Kama ilivyo kwa ziwa Victoria, tuna Ziwa Nyasa na Mji wa Tukuyu hauna maji, ni lini Serikali italeta fedha kuhakikisha maji yanatoka Ziwa Nyasa Hadi kufika Tukuyu?
Akijibu swali hilo Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema Moja ya mikakati iliyopo Serikalini ni kuhakikisha rasilimali zilizopo nchini zinatumika na kutatua changamoto za wananchi.
"Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Moja ya mikakati na maelekezo ni kuhakikisha rasilimali zilizopo nchini zinatumika na kutatua matatizo ya maji,kwa hiyo maeneo ya Ziwa Nyasa ni moja ya mikakati ya Wizara ,na Wizara ipo katika hatua mbalimbali kufanya 'visibility Study' ,naamini wananchi wa maeneo hayo pia watanufaika kupata Huduma ya maji safi na salama."amesisitiza Aweso
No comments:
Post a Comment