
MBUNGE wa Viti Maalum Husna Sekiboko amehoji hatua zinazochukukiwa na Serikali Ili kulinda Kilimo Cha matunda kwa lengo lai kuokoa soko la matunda linalosuasua kutokana na uingizaji mkubwa wa matunda nchini.
Akiuliza swali Bungeni Sekiboko pia amesema "Mkoa wa Tanga ni maarufu kwa Kilimo cha matunda hasa machungwa lakini bado hayajapati soko zuri kwenye viwanda,ni upi mkakatii wa Serikali katika kuboresha Kilimo Cha matunda ili kuweza kukidhi mahitaji ya viwandani?amehoji Sekiboko na kuongeza kuwa
"Pamekuwa na changamoto kubwa ya kuoza matunda kabla ya kufika sokoni ,ni upi mkakati wa Serikali wa kujenga vyumba baridi kwa ajili ya kuhifadhi matunda ."
Akijibu maswali hayo ,Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amesema katika kulinda soko na kudhibiti uingiaji holela wa matunda nchini, Serikali imechukua hatua mbalimbali zikiwemo kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) ambayo itaweka utaratibu wa kuwezesha uingizaji na usafirishaji nje wa mazao ya nafaka na mazao mchanganyiko yakiwemo matunda.
"Pia imeamasisha uanzishaji wa viwanda vya kusindika matunda ili kuimarisha soko la ndani na kupunguza upotevu,kutoa ruzuku ya pembejeo kwa mazao ya matunda ikiwemo maembe, machungwa na parachichi ili kuongeza tija na kuimarisha utafiti na uzalishaji wa mbegu na miche bora ya matunda kulingana na mahitaji ya soko.
Aidha Silinde amemthibitishia Mbunge huyo kwamba Serikali, inatambua mkoa wa Tanga ni Moja ya Mkoa unaotegemewa kwa Kilimo cha machungwa .
"Tunakiri kwamba kuna changamoto kubwa ya kuoza kwa matunda hayo ambayo imekuwa ni Moja ya jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali kuokoa matunda hayo ambapo kazi kubwa iliyofanyika sasa hivi ni kuhamasisha sekta Binafsi kuingia katika kujenga viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao haya kama vile Kutoka katika tunda kuwa juisi na Tanga ndio mkoa ambao sasa hivi tumeuweka kwenye mkakati huo."amesema Silinde
Kuhusu kuoza mazao amesema,Serikali inao Mpango madhubuti na tayari imepata fedha kwa ajili ya kujenga vyumba baridi kwa ajili ya kuhifadhi haya matunda
No comments:
Post a Comment