DECOHAS yajivunia mafanikio kutokana na mazingira mazuri ya Uwekezaji nchini

PICHANI kushoto Afisa Habari na Mahusiano wa DECOHAS Nicholaus Lwena na kulia ni Makamu Mkuu wa DECOHAS  ,Taaluma,Utafiti na Uelekezi,Dkt.George Adriano

 

   NA JOYCE KASIKI,DODOMA

MAKAMU  Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi    (DECOHAS)  ,Taaluma,Utafiti na Uelekezi,Dkt.George Adriano ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya Uwekezaji ambayo yameweza chuo hicho kufanya uwekezaji wenye tija kwa wananchi hususan vijana na Taifa kwa ujumla .

Akizungumza na waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya chuo hicho yaliyopo Nala jijini Dodoma  ,kuhusu  sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya DECOHAS yatakayoambatana na mahafali ya saba ya chuo hicho tangu kuanzishwa kwake 2010

,Dkt.Adriano amesema kutokana na mazingira ya Uwekezaji kuboreshwa,chuo hicho kimeweza kutanua wigo  wa utoaji wa huduma zake katika kada ya Afya kwa wanafunzi wengi zaidi kwa Sasa tofauti na kilipoanzishwa .

"Nachukua nafasi hii kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya Uwekezaji ."

Ameitumia nafasi hiyo kuiomba Serikali iendelee kuwa pamoja nao na kuwaamini kwamba kinatoa taaluma bora ambayo huwawezesha wahitimu kuchangia katika utoaji wa huduma za Afya Serikalini na binafsi katika vituo vya Afya maeneo mbalimbali  hapa nchini.

Awali ,Afisa Habari na Mahusiano wa chuo hicho,Nicholaus Lwena amesema katika kipindi Cha miaka kumi sasa DECOHAS  kinajivunia kuisaidia serikali katika kutoa elimu ya afya ambapo toka kuanzishwa kwake kimeshatoa wahitimu zaidi ya 4000 katika kada mbalimbali za Afya.

Lwena amesema katika mahafari ya  Saba yanayotarajiwa kufanyika Desemba 15,2023 ,wahitimu   700 watatunukiwa vyeti . 

Aidha amesema  katika muongo huo mmoja chuo kimejipambanua vyema katika kutoa elimu bora na watu wenye weledi wa hali ya juu katika fani zote zinazotolewa chuoni hapo.

"Kwasasa chuo kina wanachuo zaidi ya 3000  na wanachuo 4944 waliomaliza hapa tangu kuanzishwa kwake ambao wengi wao wapo katika soko la ajira serikalini na sekta binafsi,"amesema Lwena

Aidha Lwena amesema kuwa wamekuwa wakisimamia taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa jamii kwa kutoa huduma ya matibabu ya uhakika kwa wagonjwa kwenye kwenye hospitali zao na baadhi ya wengine wamekuwa wakipata huduma bure kutokana na changamoto za kifedha na sababu zingine mbalimbali.

"Chuo kimekuwa kikishiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii mfano kuchangia damu safi na salama kwa jamii na taasisi ya damu salama,kupima baadhi ya vipimo na kutoa ushauri wa matibabu bure kwenye jamii inayotuzunguka,maonesho mbalimbali,"amesema Lwena.

Vile vile  amesema kuwa chuo kinatambua wanachuo wenye changamoto za ada hivyo kuna zaidi ya wanachuo 16 wanasoma bure chuoni hapo kwa kufadhiliwa na chuo kila kitu.

"Ndiyo maana leo tumeamua kufanya tukio kubwa la kihistoria katika maadhimisho ya miaka 10 ya mahafali ya saba ya DECOHAS ambapo tumemualika msanii wa kizazi kipya   Rayvany kutumbuiza katika sherehe yetu,"amesema Lwena

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.