Shekimweri afungua Kongamano la maadhimisho ya sikubua Takkwmu Afrika


 Na Joyce Kasiki, Dodoma

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amefungua Kongamano la maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika yaliyobebwa na kauli mbiu isemayo uboreshaji wa mifumo ya ushirikiano wa kitakwimu ili kuharakisha utekelezaji wa eneo huru la biashara la Afrika(AFCFTA)mchango wa Takwimu rasmi na'big data'katika mageuzi ya kiuchumi na maendeleo endelevu ya afrika.

Akifungua Kongamano hilo Mkuu huyo wa wilaya amesema,Ofisi za Taifa za Takwimu Barani Afrika hazina budi kuendelea kuzalisha takwimu rasmi ,zenye ubora na kuzisambaza kwa wakati Ili kuiwezesha Serikali kufanya maamuzi hasa katika eneo la kuleta maendeleo ya watu kwa wakati Barani Afrika

Kwa maananhiyo Ofisi za Taifa za Takwimu hazina budi   kuboresha mifumo ya ushirikiano wa kitakwimu ili Takwimu ziweze kuwafikia wadau kwa urahisi na  na kwa kuzingatia matumizi ya njia rahisi za usambazaji wa Takwimu husika.

Kwa mujibu wa  Shekimweri Ofisi za Taifa za Takwimu barani afrika zinawajibu mkubwa wa kusaidia Nchi kufanya maamuzi yanayohusu sera kuhusiana na eneo huru la biashara afrika.

" Takwimu zinakuwa na maana pale ambapo zinatolewa taarifa kwani zinakwenda kukidhi mahitaji kwa usahihi na idadi husika ya watu."

Akizungumza katika Kongamano hilo Kaimu Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu NBS Emilian Karugendo 

amesema kuwa matumizi ya Takwimu rasmi ndio msingi wa kila kitu katika maisha,katika mipango na katika kufuatilia programu mbalimbali na utekelezaji wake.

Karugendo ametaja mada za Kongamano hilo kuwa ni pamoja na   uboreshaji wa mifumo ya ushirikiano wa kitakwimu ili kuharakisha utekelezaji wa eneo huru la biashara la Afrika(AFCFTA),mchango wa Takwimu rasmi na'big data' katika mageuzi ya kiuchumi na maendeleo endelevu ya Afrika.

Ametaja mada  nyingine ni matokeo ya sensa ya watu na makazi mwaka 2022 na mwongozo wa kitaifa wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 na matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yanawezaje kutumika kwa pamoja na matokeo ya tafiti nyingine ili kuongeza matumizi na thamani ya Takwimu rasmi katika sekta ya kilimo nchini.

Naye Mhadhiri chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika  Godfrey Saga  amesema  lengo kubwa la kongamano hilo ni kuweka ufahamu katika tasnia  ya Takwimu kuanzia shughuli za ufundishaji masuala ya utafiti na masuala ya ushauri wa kitaalamu pamoja na kutumia taarifa hizo zinazotokana na takwimu mbalimbali.


Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.