MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akisalimiana na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt.Albina Chuwa katika viunga vya Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma. |
BAADHI ya wadau wa Takwimu waliofika katika maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika jijini Dodoma |
Na Joyce Kasiki,Dodoma
MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Dkt.Albona Chuwa amewataka watakwimu katika sekta mbalimbali kufanya kazi ya ziada ya kuwapatia ViongozI wao takwimu sahihi zizlizopata kibalo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ili waweze kuzitumia katika kuleta maendeleo ya watu na Taifa kwa ujumla.
Dkt.Chuwa ametoa kauli hiyo leo Nov 21,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya 33 ya siku ya Takwimu Afrika .
“Watakwimu wa Halmashauri, Wizara, Idara naTaasisi za umma mnapaswa kufanya kazi ya ziada kwa kuwapatia viongozi wenu takwimu sahihi ambazo zimepata kibali kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu pale wanapowasilisha taarifa kwa wananchi au viongozi wa juu ili kuepuka upotoshaji wa takwimu.”amesema Chuwa
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo ameelezea umuhimu wa Takwimu huku akisema ,Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotoa Takwimu bora na zinazoaminika ulimwenguni .
Senyamule ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa Ofisi ya Takwimu hapa nchini (NBS) kusambaza taarifa za kitawimu kwenye Halmashauri hapa nchini kwani Takwimu zinatakiwa kutumiwa kwenye kutafsiri mipango ya maendeleo kwa sekta zote.
Aidha amesema Takwimu zinasaidia nchi za Afrika kufahamu idadi ya rasilimali watu iliyopo na makundi yake.
Kwa upande wae Kamisaa wa Sensa Zanzibar Balozi Mohamed Ally Hamza amesema maadhimisho hayo yamelenga kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu matumizi ya sensa pia ushirikishwaji wa jamii unasaidia kuongeza thamani ya Takwimu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment