Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha kujenga uwezo kwa Kamati za Usimamizi wa Maafa Mkoa wa Lindi kuhusu hatua za kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa wakifuatilia mada wakati wa kikao hicho. |
NA. MWANDISHI WETU
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na
Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amezihimiza Kamati za maafa nchini
kuendelea kuweka mikakati Madhubuti katika kuzuia, kujiandaa na
kukabiliana na maafa pindi yanapotokea.
Ameyasema
hayo Mkoani Lindi alipokuwa akifungua kikao kazi cha kujenga uwezo kwa
Kamati za Usimamizi wa Maafa Mkoani humo kuhusu hatua za kuzuia,
kujiandaa na kukabiliana na maafa kilichoratibiwa na Idara ya
Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo kimelenga kuifikia
mikoa katika kuzijengea uwezo kamati hizo katika ngazi zote.
Naibu
Waziri huyo amezikumbusha Kamati hizo umuhimu wa kujiandaa na
kukabiliana na maafa kwa kuzingatia madhara yatokanayo na maafa.
“Kikao
kazi cha leo kimezingatia wajibu mlio nao kwa mujibu wa Sheria ya
Usimamizi wa Maafa namba 6 ya Mwaka 2022 na Kanuni zake, ambayo
imeanzisha Kamati za Usimamizi wa Maafa za Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji
au Mitaa. Jukumu la msingi la Kamati hizi ni kuchukua hatua kwa lengo
la kuzuia na kupunguza madhara ya majanga ya aina zote na kujiandaa
kukabili na kurejesha hali kwa ubora zaidi endapo maafa yatatokea,”
alieleza.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwakumbusha
wajibu wa kila mmoja katika eneo lake la kazi kuendelea kuchukua hatua
stahiki endapo maafa yanatokea huku akieleza kuwa mfumo wa Serikali
umezingatia wajibu wa sekta na taasisi yenye jukumu kisera na kisheria
kuchukua hatua ili kuokoa maisha na mali za jamii yetu kutokana na
matukio ya maafa.
“Uzoefu unaonesha kuwa kuchukua
hatua za mapema za kuzuia na kupunguza madhara zimekuwa na gharama nafuu
kuliko kusubiri ili kuchukua hatua baada ya maafa kutokea ambapo,
serikali imekuwa ikilazimika kutumia fedha nyingi, hivyo tuendelee
kujipanga mapema,” alisisitiza
Mhe. Nderiananga
alikumbusha kuwa hatua hii ni muhimu ili kuhakikisha juhudi
zinazochukuliwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, katika kuimarisha uchumi na huduma za kijamii
katika ujenzi wa Taifa letu zinakuwa stahimilivu dhidi ya maafa.
“Ni
dhahiri kuwa hatua mnazochukua zitachangia katika juhudi zake katika
kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango ya Serikali pamoja na
maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025 kwa
manufaa makubwa kwa wananchi na tija iliyokusudiwa,” alisema Naibu
Waziri huyo.
Akitoa salamu za Mkoa kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe Shaibu Ndemanga
amesema mkoa umeendelea na jitihada za kujiandaa na madhara yanayoweza
kutokea kutokana na maafa huku ikiendeelea kujipanga na mvua
zinazoendelea kunyesha nchini kwa kuzingatia utabiri wa Mamlaka ya Hali
ya Hewa ya uwepo wa Mvua za El nino na kuahidi kutekeleza maagizo na
maelekezo yaliyotolewa kwa kuzingatia umuhimu wa tahadhari za mapema.
No comments:
Post a Comment