Mavunde aonya utoroshaji wa Madini

 


 

Na Joyce Kasiki,Dodoma


WAZIRI wa Madini Anthony mavunde wamewaonya  wadau wa madini kutojihusisha na utoroshaji wa madini nchini huku akisema kuwa, atakayebainika atachukuliwa hatua Kali  za kisheria ikiwemo kufutiwa leseni katika maeneo yote ambayo muhusika anafanya shughuli zake za madini  hapa nchini.

Mavunde ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa chama cha Mabroka katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma huku akisema wadau hao wanapaswa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha  seta ya madini inawanufaisha watanzania na Taifa kwa ujumla.

“Nataka niwahahakikishie  kwamba najua michezo hii inafanyika sana katika mkoa wa Morogoro na ninafahamu, mliniona juzi Kahama nilifika usiku kwenye utoroshaji ,na niwape salamu tu,hao ambao wanakiuka utaratibu watanikuta huko ,na Mimi staili yangu ni moja tu maana Sheria inasema vizuri na mimi nipo hapa kwa mujibu Sheria, unakiuka masharti ya leseni naupa ‘suspension’ sijiulizi mara mbili nasimamisha leseni,kwa hiyo Katibu Mkuu naamini hilo tutalisimamia vizuri.”

Ameomba ushirikiano kutoka kwa wadau hao kuhakikisha wanashirikiana na Serikali Ili kukuza sekta ya Madini hapa nchini Ili kufikia lengo lililowekwa na Serikali la kutaka sekta hiyo ikusanye kiasi Cha shilingi Trilioni Moja .

“Hili linahitaji ushirikiano na uadilifu katika sekta hii,tushirikiane kuhakikisha rasilimali hii inatufaisha,ninyi ndio wadau wakubwa mtakaotusaidia katika hili la utoroshaji maana nyie ndio mnaowapelekea madini ,kwa hiyo mnawafahamu,msinikwaze kwa kushirikiana na ‘dealers’ kutorosha madini na nikimkamata mmoja nafuatilia mnyororo mzima simuachi hata mmoja,

“Hivi tunavyozungumza kuna watu nimewashikilia Chunya na Geita na mtawaona mahakamani muda si mrefu ,baada ya maamuzi ya mahakama na ikatoa  maamuzi ya kwamba umethibitika nafuta leseni na ninaku-‘black list’ hufanyi tena biashara ya madini.amesema Mavunde na kuongeza kuwa

“Juzi nimekwenda Kahama nimekuta mzigo wa kilo 4.3 wenye thamani ya shilingi milioni 562 nimesimamisha leseni ya muhusika,na sasa hivi nikikuta unatorosha madini kwanza nasimamisha leseni zako nchi nzima wakati tunasubiri uamuzi wa mahakama,nawaomba kama hii ndio biashara yako fuata Sheria tukifanya hivyo tutaisaidia nchi yetu.”

Waziri Mavunde amewaasa wadau hao kutoa maoni yao ama unahitajika kufanyika marekebisho ama katika  sera au  sheria za madini Ili kuwawezesha kufanya biashara ya madini na kuisaidia serikali katika kukusanya  mapato na siyo kutorosha madini.

“Nimesema milango ipo wazi njoo uniambie tatizo lipo wapi ili tuboreshe na kufanya marekebisho yatakayowawezesha kufanya biashara ya Madini bila udanganyifu.”

 Awali Mwenyekiti wa CHAMMATA  Jeremia Kituyo ameeleza changamoto zinazoikabili CHAMMATA  ambapo amesema ni pamoja na leseni kukatwa kila mkoa,baadhi ya madini kama Tanzanite kuzuiwa kuuzwa katika mikoa mingine,Mabroka kukosa mikopo katika taasisi za kifedha ,wageni kusogelea maeneo yao ya uchimbaji hasa katika maeneo ya Maganzo,Mahenge na Mererani .
Aidha ametaja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa  zahanati ndani ya ukuta wa Mererani.

Ametumia nafasi hiyo kuishauri Serikali kurudisha soko laadini Mererani lakini pia kuangalia upya suala.la ukataji leseni na kwamba badala ya kukatwa kila.mkoa basi leseni zikaywe kwa Kanda.

Kwa mujibu wa Kituyo kitendo cha Tanzanite  kuuzwa Mererani pekee yake kimedororesha biashara ya madini .
"Kwa.mfano soko la Arusha ni la kitaifa linapokea madini kutoka mikoa yote  nchini,sasa kitendo Cha Tanzanite kuzuiwa kuuzwa mikoa mingine kimefifisha biashara."amesisitiza Kituyo

Ametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali kuiachia Tanzanite iendee kuuzwa katika masoko huku wakiithibitishia Serikali liyalibda madini hayo.

xxxxxx

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.