Meneja Mkuu wa Mgodi wa Kampuni ya Franone MiningVitus Ndakize |
Na Mary Margwe, Geita
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Kampuni ya Franone MiningVitus Ndakize amesema kuwa kampuni hiyo iliyoanza tangu mwaka 2011 imekuwa na rekodi ya kutoka katika uchimbaji mdogo hadi kufikia uchimbaji wa kati.
Ndakize anatumia fursa yake akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari kwenye maonesho hayo na huku akiishukuru Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kwa miongozo na maelekezo kwa wachimbaji wadogo kupiga hatua kutoka uchimbaji mdogo na kuwa wachimbaji wa kati na hatimaye kuwa mchimbaji mkubwa.
" Kutokana na jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan alizozifanya kwenye Sekta ya Madini tumeweza kuinuka wachimbaji kutoka uchimbaji mdogo hadi kufikia uchimbaji wa kati, hivyo tunamshukuru sana mama yetu, Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan" anasema Ndakize.
Akieleza mipango ya Kampuni amesema kuwa wamejiwekea kukua zaidi na kutengeneza ajira nyingi kwa Watanzania pamoja na kuendelea kuongeza migodi katika Mikoa mingine, ambapo anaongeza kuwa wana Ofisi katika Mkoa wa Manyara na Morogoro .
No comments:
Post a Comment