Na Renatha Msungu,Dodoma
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Tanzania Chesire Foundation,limefanikiwa kuwafikia watoto zaidi ya 2800 kutoka katika mikoa ya Dodoma na Shinyanga katika utekelezaji wa mradi wa elimu jumuishi katika shule za msingi.
Hayo yamesemwa na mhasibu wa mradi Kutoka Tanzania Chesire Foundation Anna Pusse katika maonyesho ya wiki ya taasisi zisizo za kiserikali yanayoendelea katika viwanja vya Jakaya Kikwete vilivyopo jijini Dodoma.
Pusse amesema lengo la mradi Jumuishi katika mikoa hiyo ni pamoja na kuwainua watu wenye ulemavu kielimu na kiuchumi, lakini pia kuwasaidia kutotengwa na jamii nyungune.
“,Mradi wa elimu Jumuishi katika mikoa hiyo,umesaidia kwa kiasi kikubwa, kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata elimu wakiwa wamechangamana na watoto wa kawaida, nah ii imesaidia jamii hiyo kujiona sawa na wengine,”amesema Nguse.
Pusse amesema kwa upande wa shinyanga mradi wa elimu Jumuishi unatekelezwa katika shule za msingi 47 ambapo umeonyesha mafanikio makubwa kutokana na mwitikio ulioonyeshwa na wazazi kwa kuwaleta watoto katika shuke kupata elimu.
Pusse amesema wito wake kwa serikali ni pamoja na kuwataka kuendelea kuisisitiza jamii kuhakikisha inawapeleka watoto wenye ulemavu shuleni kwa ajili ya kupata elimu.
Anasema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni pamoja na watu kuwa na uwelewa mdogo ya kuwa hata watu wenye ulemavu wanahaki ya kusoma kama ilivyo jamii nyingine.
Naye Enock Isaya mmoja wa wanufaika wa mradi wa elimu Jumuishi anasema hakuna sababu ya kuwaficha watoto wenye ulemavu,badala yake wawatoe ili waende kupata elimu jumuishi, kwa sababu serikali hivi sasa imewekeza kwenye elimu, ikiwemo kuongeza bajeti.
Naye Mwita Marwa amesema mradi wa elimu jumuishi una umuhimu mkubwa hivyo wazazi wanapaswa kutoa Ushirikiano pale watoto wenye ulemavu wanapotakiwa kwenda shuleni, wawapeleke.
No comments:
Post a Comment