Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akizungumza na wamiliki wa shule nchini |
Na Joyce Kasiki,Dodoma
WIZARA ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia imekutana na wamiliki wa shule nchini kwa lengo la kujua namna wanavyofanya kazi lakini pia kufahami changamoto zinazoikabili.
Akizungumza Leo jijini Dodoma katika mkutano na wamiliki hao wa shule zisizo za Serikali Waziri wa wizara hiyo Prof.Adolf Mkenda amesema kundi hilo ni muhimu kwa Serikali na sekta ya Elimu kwani linachangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya Elimu.
Amesema wadau hao wameongeza fursa Kwa wazazi kuchagua wapi watoto wao waende kusoma licha ya changamoto zilizopo ambapo Serikali inaendelea kuzitafutia ufumbuzi.
Akizungumza kuhusu mitaala mipya inayotarajiwa kuanza kutumika Januari 2024,Waziri huyo amesema mageuzi hayo yameshirikisha watu wengi kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kwamba watu wasikilizwe Ili kuleta tija katika mitaala na sera mpya ambayo ipo katika hatua za mwisho Ili ianze kutumika.
Amesema mapendekezo yaliyopo Elimu ya lazima ni miaka kumi ambapo ni darasa la.kwanza hadi darasa la sita na kidato cha kwanza hadi kidato cha nne,Kisha mtoto ataendelea kidato Cha Tano na sita kama atachaguliwa na baadaye kwenda chuo Kikuu.
Aidha amesema ,mitaala hiyo ambayo inatarajiwa kuanza Januari 2024,haitaanza kwa mkupuo na badala yake itaanza na baadhi ya madarasa Ili kumudu mabadiliko yaliyopo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omari Kipanga amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kusikiliza ili Serikali ifahamu changamoto ambazo zinawakabili na kuweza kukaa pamoja kuzijadili na kutafuta namna Bora ya kuzitatua.
"Lengo letu kuu ni kusikiliza ili tupate kufahamu changamoto mnazokabiliana nazo lakini tuweze kukaa Kwa pamoja kujadili changamoto hizo na kutafuta namna Bora ni namna gani tunaweza kutatua changamoto lakini namna gani tunaweza kushirikiana na Wafanyakazi Kwa pamoja ndio lengo la kikao hiki,"alisema Naibu huyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi amesema kuwa katika maandalizi ya Taifa lolote iwe kiuchumi,elimu ni lazima kijana aandaliwe vizuri ili awe tegemeo Kwa Taifa.
"Katika maandalizi mazuri ya Taifa lolote katika masuala ya kiuchumi na kielimu ni lazima kijana aandaliwe vizuri kwakuwa tunaowajibu huo wa msingi Kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali kuweza katika kuhakikisha kunakuwa na sera bora lakini pia sheria na utekelezaji mzuri wa majukumu ambayo kimsingi Serikali itimize wajibu wake wa kutoa mazingira wezeshi kwa vijana ambao wanazaliwa katika Taifa hili,
Kwa sehemu kubwa katika sekta ya elimu ndio tunawatu wengi zaidi na huko ndiko tunakokwenda kupata Taifa ambalo ni endelevu na lenye kizazi ambacho kinaandaliwa vizuri ili kuweza kupata kama ni wafanyabiashara watakuwa bora sababu ya misingi ya elimu ambayo Wizara ya elimu inaiandaa,"amesema.
No comments:
Post a Comment