Siku ya Mwanamke anayeishi kijijini yaleta neema Olivolos

        

        Na Mwandishi Wetu.      

 Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dr Dorothy Gwajima amewaagiza maafisa maendeleo nchini kuongeza kasi ya kufikia makundi yote ya wanawake wajasiriamali hasa waishio vijijini na kupokea changamoto zinazowakabili na mapendekezo yao ili kuweka mikakati ya kuwezesha kila kundi la mwanamke kufikia mbele zaidi kimaendeleo.

"Ni wakati sasa maafisa maendeleo ya jamii kufanya sensa ya hizi changamoto tujumuishe ya kiwizara tuyajue, ya kimkoa tuyajue ya kiwilaya tuyajue na mpaka ya kwenye ngazi ya chini", Amesema Waziri Dr Gwajima. 

Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia katika maadhimisho ya siku ya mwanamke anayeishi kijijini Tarehe 15, Oktoba 2023.  yenye kauli mbiu Wezesha wanawake wanaoidhi kijijini kwa uhakika wa chakula lishe na uendelevu wa familia, ambapo kitaifa yalifanyika katika Mkoa wa Arusha, Wilaya ya Arumeru kijiji cha Olivolos. 

Aidha amewahasa wananwake kuendelea kujiunga na majukwaa ya sekta mbalimbali za uwezeshaji wanawake kiuchumi ili kupata fursa za kukutana na wanawake mbalimbali na kujigunza namna ya kutatua changamoto zinazowakabili na adhima yao ya kujiendeleza, ambapo majukwaa hayoni rahisi kufikiwa na Afisa Maendeleo. 

Hata hivyo Waziri Dr Gwajima amesistiza wanawake wajasiriamali kuendelea kuboresha bidhaa na vifungashio katika bidhaa zao huku akiwahasa kushiriki maonyesho mbalimbali ili kutoka kuona wanawake wengine wanafanya nini.

"Na hapa mazingira mazuri yamewekwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuwajengea uwezo wanawake katika kuboresha vifaa na vifungashio pamoja na kuwaunganisha na taasisi za viwango vya bidhaa ili kukuza na kutumia teknolojia sahihi rahisi ya uzalishaji", Amesema Waziri Dr Gwajima. 

 Halikadhalika Dr Gwajima amesema kuwa ni vema wanawake wajasiriamali kujikita katika  kutumia  mitandao ya kijamiii kibiashara ili kusimama na ulimwengu wa kidigitali.

"Fungua ukurasa mitandaoni ya kidigitali, business card hawana tubadilike dunia hii ukiweka kitu mtandaoni kinaangaliwa na watu elfu moja siku hiyo jiyo wakati wewe watu elfu moja dukani kwako kwa siku hawawezi kuja", Amesema Waziri Dr Gwajima. 

Sambamba na hayo yote Waziri Dr Gwajima amesisitiza kuendelea kumlimda mtoto ili kupungiza ukatili kwa watoto, huku akisisitiza familia kuwa kitovu cha kwanza kwa kumjengea mtoto maadili mema.

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.