TUCTA wakielewa kikotoo Cha asilimia 33 ,wampongeza Rais Samia






NA JOYCE KASIKI,DODOMA

SHIRIKISHO la Vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA) limempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha dhamira ya dhati ya kumkomboa mtumishi wa Umma mara baada ya kukoma utumishi wake kwa kuweka kikokotoo kipya cha mafao ya wastaafu cha asilimia 33.

Mbali na hilo Baraza hilo limempongeza Ras Samia kwa kuwapa semina baraza hilo kuhusu kikokotoo hicho kipya ili kuwajengea uelewa kwa ajii ya kufikisha elimu hiyo kwa wafanyakazi wote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mara baada ya kuhitimishwa kwa kikao cha Baraza hilo kilicholenga kuwajengea uelewa kuhusu sheria mpya ya mafao,Mjumbe wa Baraza Kuu la TUCTA Emmanuel Mwakajila amesema,wao kama wawakilishi wa wafanyakazi wameona sheria hiyo ni nzuri na wataelimisha wafanyakazi wote waielewe.

“Kama mtakumbuka Mei mosi mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan , alitangazia umma wa wafanyakazi kwamba amekubali ombi la wafanyakazi kufikia kikokotoo cha asilimia 33 wakati wanapostaafu na kuachana na kikokotoo cha asilimia 25.”amesema Mwakajila

Mwakajila amesema,hatua hiyo ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Baraza la TUCTA,ni ya kupongezwa kwani itatumika huku wafanyakazi wakiwa wanaielewa vizuri.

“Kuna na upotoshaji ambao umezagaa kwamba kikokotoo hicho kinaenda kunyonya na kunyonga haki za watumishi,lakini kwa semina ambayo imetolewa kwetu imeonyesha dhahiri dhamira njema ya serikali iliyopo madarakani ya kuhakikisha kwamba mstaafu anapostaafu kila mwisho wa mwezi atakuwa anapokea kiasi kikubwa cha pensheni tofauti na kikootoo cha asilimia 25 kinachotumika sasa.”amesema na kuongeza kuwa

“Hii inaweka uhakika wa maisha ya mtumishi wa umma mara baada ya kustaafu..,lakini kwa muda mrefu vikokotoo hivi vilikuwa havitendi haki kwa maana kikokotoo cha zamani cha asilimia 25 kilikuwa kinawapa faida watu wachache ambao walikuwa wakipata asilimia 50.”

Amesema, kwa sheria na kanuni hiyo mpya watumishi wa sekta zote wanaenda kufurahia mafao ya usawa huku akisema hilo ni takwa la kikatiba la kikatiba la kuhakikisha kwamba sheria za nchi zinazotungwa zinakuwa ni zile zinazozingatia usawa.

“Lakini kikokotoo cha asilimia 25 kwa mtaalam yeyote ataona kwamba huo ulikuwa ni ubaguzi katika suala zima la ajira na vikokotoo kwamba wote wanachangia sawa lakini huyu mmoja analipwa kwa asilimia 25 na mwingine analipwa kwa asilimia 50.”amesisitiza Mwakajila

Amesema,licha ya kuweka mfumo wa malipo sawa kwa wastaafu katika utumishi wa umma lakini kwa kanuni hiyo mpya ya kikokotoo inaenda kuweka uhimilivu wa mfuko na hivyo kuleta afya ya mfuko na uhakika kwa watumishi kuweza kunufaika na mafao.

Vile vile amesema,kanuni hiyo mpya ya mafao inaenda kuruhusu mtumishi kabla hajastaafu aweze kupata mikopo ya ziada ili aanze kuandaa makazi yake,lakini pia baada ya kustaafu atakuwa anapata pensheni ya mwezi sawa na mshahara wake wa mwisho aliokuwa anaupata.

“Kwa hiyo unaona kwamba kuna uhakika mkubwa ,na Rais Samia ameingia madarakani na kukuta mifuko hiyo ikiwa na madeni makubwa lakini amekuja kulipa zaidi ya shilingi bilioni 700 ili kunusuru hali ya mifuko “amesema Mjumbe huyo

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.