AFISA Mradi,Mradi wa Mtoto kwanza Magret Mukama akifafanua jambo katika kikao kazi cha wadau kuhusu utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ( MMMAM) kilichofanyika jijini Dodoma |
MATUKIO katika picha ni baadhi wadau walioshiriki katika kikao kazi hicho. |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
SHIRIKA lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na
masuala ya Malezi na Makuzi ya Watoto ‘Action for Community Care
(ACC)’limewakutanisha Maafisa Maendeleo ya Jamii,Maafisa Ustawi na viongozi wa
Dini kutoka wilaya zote nane za Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuweka mpango kazi
wa pamoja katika utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo
ya Mtoto (PJT-MMMAM) ya mwaka 2021/22-2025/26 hadi katika ngazi ya jamii.
Akizungumza wakati wa kikao kazi cha kuandaa mpango
kazi huo Afisa Mradi katika Mradi wa Mtoto kwanza Magret Mukama amesema,kwa
kuwakutanisha wadau inakwenda kuchochea utekelezaji wa Programu hiyo na
hatimaye kujenga watu ambao watakuwa na tija katika Taifa.
“Serikali
inatekeleza Programua ya Taifa ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto
ya Miaka mitano kwa kushirikiana na wadau mbalimbali,kwa hiyo leo
tumewakutanisha wadau hawa tuweze kuwapitisha katika Mwongozo wa PJT-MMMAM nao
waielewe na hatimaye waweze kufikisha elimu hii katika jamii kila mmoja kwa
nafasi yake.”amesema Mukama
Wakizungumza katika kikao kazi hicho viongozi wa
dini wamesema,Progframu hiyo imekuja kwa wakati muafaka na wao kama viongozi wa
dini watatuia nafasi zao kuhakikisha elimu inafika kwa jamii ambayo ni waumini
wao.
Kuhani Raha Halisi wa Kanisa halisi la Mungu Baba
la wilayani Kondoa amesema,kwa kutumia nafasi zao watahakikisha ujumbe wa
Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Mtoto unafika kwa waumini kupitia nyumba zao za
ibada.
“Sisi viongozi wa Dini tuna watu wengi na
tunaaminika,kwa hiyo hili jambo limekuja kwa wakati muafaka na sisi
tutahakikisha tunashirikiana na Serikali katika utekelezaji wa suala hili ili
watoto wapate malezi ambayo yatawafanya wakue vyema na baadaye kuleta tija
katika Taifa.”amesema Kuhani huyo
Afisa Ustawi wa Jamii Elizabeth Shoo kutoka wilaya
ya Kondoa amesema,wakati wa utekelezaji wa Programu hiyo utakidhi haja na
kurejesha msingi wa malezi na makuzi ya watoto.
“Siku hizi na huu utandawazi uliopo kila mtu
amekuwa ‘busy’ wazazi wamejisahau jukumu lao la malezi wameliacha kwa wasichana
wa kazi,u-busy wa kutafuta pesa umefanya wazazi hawajui hata kuhusu ulinzi na
usalama wa watoto wao,lakini kwa ujio wa Programu hii sasa wazazi watakwenda
kuamka na kulea watoto kwa kufuata misingi iliyowekwa na kuwawezesha kukua kwa
utimilifu wao.”amesema Shoo
No comments:
Post a Comment