Wanufaika 640 wa Samia scholarship kugharimu sh.3 bilioni

 

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknlojia Profesa Adolf Mkenda 

NA JOYCE KASIKI,DODOMA

WAZIRI  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema ufadhili wa 'SAMIA SCHOLARSHIP' una thamani ya shilingi   bilioni 3 Huku akisema katika ufadhili huo ,Serikali itagharamia kwa asilimia (100%) masomo ya chuo Kikuu kwa wanafunzi ambao wamepata udahili katika fani za Teknojia,Uhandisi,Hisabati na Tiba huku wanafunzi 640 wakichaguliwa katika ufadhili huo.

Akizungumza leo Septemba 27,2022  jijini Dodoma Profess Mkenda amesema ufadhili huo no maalum kwa ajili ya wanafunzi wa kidato Cha sita waliopata ufadhili wa juu katika mtihani wa Taifa mwaka 2022.

Amesema mwanafunzi mwenye sifa ya kupata ufadhili huo ni yule ambaye amepata udahili katika katika programu za Sayansi, teknolojia, uhandisi, Hisabati au tiba katika chuo kikuu hapa nchini kinachotambuliwa na Serikali ambazo zimetajwakatika kundi la kwanza (Cluster) katika mwongozo wa utoaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2022/2023.

"Ufadhili huu ni kwa vyuo vya hapa nchini lakini pia ni kwa wale wanafunzi waliopata udahili katika tahasusi zilizotajwa na katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali."amesema Prof.Mkenda

Aidha amesema kuwa Ufadhili huo utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kugharamia maeneo yafuatayo ambapo ni Ada ya Mafunzo ,Posho ya chakula na malazi,Posho ya Vitabu na Viandikwa Mahitaji Maalum ya Vitivo Mafunzo kwa Vitendo ,Utafiti Vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu,Bima ya Afya na Wanafunzi watakaofadhiliwa, watagharamiwa kati ya miaka mitatu (03) hadi mitano (05) kulingana na programu husika walizodahiliwa.

"Maombi ya Samia Scholarship yatawasilishwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa njia ya mtandao https://olas.heslb.go.tz kwa siku 14 kuanzia Septemba 28, 2022." Amesema ptof Mkenda na kuongeza kuwa

"Ufadhili huu ni wa asilimia mia moja ambao kikomo chake kitazingatia miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.Orodha ya majina ya wanafunzi husika inapatikana kupitia www.moe.go.tz na www.heslb.go.tz .


UCHAMBUZI WA WANUFAIKA 640 wa SAMIA SCHOLARSHIP

Kuhusu uwiano wa kijinsia wa wanufaika 640 wa Samia Scholarship  prof.Mkenda alisema  Wasichana 244 sawa na asilimia 38% na Wavulana ni 396 sawa na asilimia 62% ambapo Wanafunzi kutoka shule za serikali ni 396 sawa na asilimia 62% wakati Wanafunzi kutoka shule za binafsi ni 244 sawa na asilimia 38%.

"Wanafunzi wenye ufaulu wa juu kiwango cha Alama tatu (3) ni 60 (9%)Wanafunzi kutoka shule za Tanzania Visiwani ni 43 (7%)Wanafunzi kutoka shule za Tanzania Bara 597 (93%)"

Aidha amesema,jumla ya wanafunzi 11 wenye mahitaji maalumu watanufaika na Samia Scholarship.Hawa ni asilimia 100 ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu waliopata darala la kwanza katika tahasusi zinazolengwa na Samia Scholarship mwaka 2022/23

Shule zilizotia fora kwa kuwa na idadi kubwa za wanufaika wa Samia Scholarship ni pamoja na Tabora Boys wanafunzi 79 (12%)St.Mary’s Mazinde Juu wanafunzi 51 (8%)Mzumbe Sekondari wanafunzi 46 (7%)Tabora Girls 39 (6%)Kisimili wanafunzi 31 (5%)

Kwa upande wake Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Abdugulam Hussein alisema kuwa ufadhili huo utaongeza chachu kwa wanafunzi wengi kusoma masomo ya Sayansi,Teknolojia, uhandisi,Hisabati na Tiba.

"Idadi iliyopo mwaka huu naamini mwakani itaongezeka sana hivyo Mhe.Mkenda kama utaweza kuongea na Mhe.Rais tena aongeze walau Bilion zingine 3 kwa mwakani ziwe 6 kwa sababu naamini idadi itaongezeka maradufu kutokana na hamasa hii,"Amesema Mhe.Ali Abdugulam Hussein 

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.