Watoto zaidi ya laki tano kuchanjwa chanjo ya polio Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule



NA JOYCE KASIKI,DODOMA

MKUU wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewaasa wazazi na walezi wenye watoto walio na umri chini ya miaka mitano kuhakikisha wanapata chanjo ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa  polio.

Akizungumza jijini Dodoma,Senyamule amesema shughuli ya utoaji chanjo mkoani humo ni ya siku nne na kwamba imeanza septemba Mosi na itahitimishwa septemba 4 mwaka huu.

Amesema kampeni hiyo ni ya nyumba kwa nyumba hivyo wazazi hawana sababu ya kuwabeba watoto na kuwapeleka vituoni kwa ajili ya kupata chanjo hiyo.

“Kampeni hii ni ya nyumba kwa nyumba hivyo wazazi na walezi watakaa nyumbani kusubiri wahudumu wa afya ambao watapita majumbani kwa ajili ya kutoa chanjo hiyo ya matone kwa watoto.”amesema Senyamule 

Amewaasa wananchi wote wa mkoa wa Dodoma waunge mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuokoa maisha ya watoto dhidi ya ugonjwa polio.

“Watoto wote wachanjwe asibaki mtoto hata mmoja ambaye hajapata chanjo,kwa kufanya hivi tutakuwa tumewaokoa watoto wetu dhidi ya mateso ya ugonjwa wa polio.”amesisitiza Senyamule na kuongeza kuwa

“Kwa hiyo tuzitumie siku hizi nne vizuri ambazo zitamwokoa mtoto dhidi ya mateso ya ugonjwa wa polio,na sisi kama mkoa tutapita maeneo mbalimbali kuona mwitikio wa wananchi katika shughuli hii.”

Kwa upande wake mratibu wa Chanjo mkoa wa Dodoma Francis Bujiku amesema,mkoa wa Dodoma unatarajia kuwafikia watoto walio na umri chini ya miaka mitano wapatao 591,624.

Aidha amesema,licha ya kuwa kampeni hiyo ni ya nyumba kwa nyumba lakini wazazi na walezi bado wanayo nafasi ya kuhakikisha watoto wanapata chanjo hiyo pindi wanapoenda kliniki au kituo chochote cha kutolea huduma za afya .

Vile vile amesema,kwa wale ambao watoto hao hawatafikiwa majumbani hadi kufikia Septemba,waende kwenye vituo vya afya na zahanati katika maeneo yao ili watoto wapate chanjo hiyo.

Afisa Programu Mpango wa Taifa wa chanjo kutoka Wizara ya Afya Lotalis Gadau amesema,awamu hii ya tatu ya chanjo ya polio imelenga kuwafikia watoto milioni 12.3 wenye umri chini ya miaka mitano nchi nzima.

Aidha akitoa matokeo ya kampeni ya chanjo  ya awamu ya kwanza iliyofanyika katika mikoa ya Ruvuma,Njombe,Mbeya na Songwe Gadau amesema,jumla ya watoto milioni 1.3 sawa na asilimia 115 walipata chanjo hiyo kutoka makadirio ya lengo la kufikia watoto 975,839 huku awamu ya pili ya kampeni hiyo ikiwafikia watoto milioni 12.1 badala ya lengo lililowekwa la kufikia watoto milioni 10.2.

 

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.