MKUU wa
mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule (katikati)akionyesha Muongozo wa Programu
Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto PJT-MMMAM
,baada ya kuizindua Prograu hiyo katika ngazi ya mkoa.
Wadau
ambao ni mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Dodoma wakimsikiliza Mkuu wa
mkoa Rosemary Senyamule katika Mkutano wa Uzinduzi wa Programu Jumuishi ya
Taifa (PJT-MMMAM) ngazi ya mkoa.
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Fatma Mganga akizungumza na wadau kuhusu Uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya MAlezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto PJT-MMMAM ngazi ya mkoa.
NA JOYCE
KASIKI,DODOMA
MKOA wa
Dodoma umezindua Programu ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya
Mtoto PJT-MMMAM huku mkuu wa mkoa huo Rosemary Senyamule akiwataka wadau wa
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kushiriki kwa dhati kutekeleza Programu hiyo
iliyolenga Taifa kuwa na watu wenye tija.
Kwa mujibu
wa muongozo wa PJT-MMMAM ,ushahidi wa kisayansi unatabiri upo uwezekano wa kudi
la watoto wenye mwanzo duni kupoteza takribani robo ya mapato ya baadaye endapo
hawatakuwa na mwanzo mzuri kuwezesha kufikia hatua timilifu za ukuaji.
Akizindua
Programu hiyo Senyamule amesema,huu ni wakati muafaka kwa jamii kujikita katika
malezi ,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwani ni eneo ambalo litaleta mabadiliko
kwa watanzania na hatimaye kupata Taifa lenye tija kwa kuwa na watu wenye uwezo
wa kufikiri mambo na kufanya maamuzi sahihi.
Amesema,maeneo
muhimu ya kuzingatiwa kwenye malezi hayo ni pamoja na Afya bora,lishe ya
kutosha,ulinzi na usalama wa mtoto ,malezi yenye mwitikio na fursa za
ujifunzaji wa awali.
“Haya ni
maeneo ambayo yakifuatwa katika kumlea mtoto atajengeka kitabia na kukuza uwezo
wake wa kufikiri mambo ,kwa mfano eneo la lishe ..,mtoto asipopata lishe ya
kutosha katika siku 1000 za mwanzo ,haimtasaidia pindi atakapokuwa mtu
mzima
“Hata
katika eneo la malezi,mtoto anapaswa apate malezi kutoka kwa wazazi badala ya
watoto kulelewa na wasichana wa kazi ,wazazi wamekuwa bize na shughuli za
kiuchumi huku watoto wakiachiwa dada wa kazi ,hii inahatarisha hata katika
suala la ulinzi na usalama wa watoto.”amesema Senyamule
Awali
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Fatma Mganga amesema,wadau waipokee programu
hiyo mpya na waifanyie kazi ili iwanufaishe watoto wa mkoa wa Dodoma na Taifa
kwa ujumla.
Afisa Maendeleo ya Jamii,Wizara ya
Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Salome Francis amesema kwa
upande wa Mikoa mpaka sasa Programu imeziduliwa kwenye Mikoa 10 ya Tabora, Morogoro,Lindi, Arusha, Manyara, Mbeya, Rukwa, Kagera na Dar Es Salaam na Mkoa wa Dodoma.
Salome amesema,Programu hiyo inatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia
mwaka 2021/22-2025/26 na inalenga kuwekeza moja kwa moja kwenye Malezi, Makuzi
na maendeleo ya Watoto wa umri wa miaka 0-8 ili kuharakisha
upatikanaji wa matokeo chanya ya Maendeleo ya Awali ya Mtoto katika utoaji wa
huduma za malezi jumuishi .
Programu ya PJT-MMMAM ,tayari
ilishazinduliwa kwa ngazi ya Taifa Desemba mwaka jana na Rais Samia Suluhu
Hassan jijini Dodoma aliyewakilishwa na Waziri wa Maendeleo ya
JamiiJinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima.
No comments:
Post a Comment