NA JOYCE KASIKI,DODOMA
TAASISI ya Mafunzo ya sheria kwa vitendo imesajili kozi ya wasaidizi wa kisheria ambayo
pia itaanza kutolewa mwaka huu hapa nchini ili kulijengea uwezo kundi hilo la
wasaidizi wa kisheria.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mkuu wa kitengo Cha sheria katika
Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria kwa Vitendo (LST) Berinda Mollel huku akisema
kozi hiyo itaanza kutolewa mwaka huu.
Vile vile Mollel amesema,wao kama wataalam wanaotoa
mafunzo ya weledi katika ngazi ya watu waliohitimu shahada ambapo wanapenda kuwa mawakili au watumishi wa umma .
“Pia tunatoa mafunzo ya weledi kwa wasaidizi wa
kisheria ,kwa hiyo jukumu letu sisi tulilopewa na nchi ni kutoa mafunzo haya
kwa sababu ndiyo taasisi pekee inayotoa mafunzo ya weledi katika ngazi hii.”amesema
na kuongeza kuwa
“Tangu kuanzishwa kituo hicho miaka 12 iliyopita tumezalisha
maelfu ya mawakili ambao wengi wao wanafanya kazi hii ya uwakili katika maeneo
mbalimbali.”amesisitiza
Mollel ametumia nafasi hiyo kuwaasa wahitimu wote wa shahada ya sheria kutoka vyuo
vinavyotambulika na Serikali wanaotarajia kufanya kazi kama mawakili binafsi
nchini au katika utumishi wa umma kufanya mafunzo ya mwaka mmoja katika
taasisi hiyo huku akiainisha kuwa wahitimu hao ni wale waliomaliza
shahada zao baada ya sheria kuanza kufanya kazi mwezi Mei 2017.
“Dhamira kuu ya taasisi hii ni kutoa ushauri
wa kisheria kwa watoto,kutoa ushauri wa kisheria kwa wanawake,kuandaa nyaraka
za mahakamani, kufuatilia mwenendo wa kesi mahakama kutoa mwongozo wa taratibu
za kufuatilia kesi, kutoa msaada wa kisheria katika makundi mengine sambamba na
usuluhishi wa migogoro”amesema Mollel
No comments:
Post a Comment