Watoto wanaoishi mazingira hatarishi watambuliwe

RAIS Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali katika hafla ya utiaji saini mkataba wa usimamizi wa shughuli za lishe .


 

           NA JOYCE KASIKI,DODOMA

RAIS Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum kuwatambua watoto wote wanaoishi katika mazingira hatarishi ili Serikali iweze kuwasaidia kwa kuhakikisha wanalelewa,wanakua vizuri na kufukia utimilifu wao ambao utaleta tija katika maisha yao ya baadaye na  Taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki Mtumba katika hafla ya utiaji saini mkataba wa lishe kwa Wakuu wa mikoa hapa nchini.

“Pamoja na kuwekeza katika suala la lishe, lakini tunafahamu kuwa wimbi la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi linazidi kuwa kubwa “amesema Rais Samia

Amesema,mwaka 2021 jumla ya watoto 992,901 walitambuliwa na kupewa huduma mbalimbali za kukabiliana na lishe duni na utapiamlo huku akihimiza kuendelea kutambuliwa kwa watoto hao ili kuimarisha afua za ukuaji wao na waweze kufikia hatua timilifu za ukuaji.

“Kuna watoto wanaishi katika mazingira magumu na kukua kwao kunakuwa kugumu hivyo hivyo, na hawa ndiyo wanakuja kuwa wahalifu wa baadaye kwa sababu kama anaishi mazingira magumu atatoka mapema nyumbani kwenda kujitafutia ,hana elimu hana namna  yoyote lakini  anakwenda kujitafutia,lazima wengi wao watakuwa wezi,watakuwa na vitendo viovu halafu tunakuja kupiga kelele.”amesema na kuongeza

“Gwajima (Waziri wa Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum) hili la kwako,mkahakikishe watoto wanaoishi mazingira magumu na hatarishi wanatambuliwa na tunawasaidia.”

Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema lishe bora ni msingi wa afya na uchumi wa mtu mmoja mmoja ambapo suala hili linapaswa kuzingatiwa kuanzia kwenye malezi na makuzi ya watoto ili kueta tija kwa Taifa.

“Lishe mbovu inaleta utapiamlo ambao unaleta madhara ya kiafya na kiuchumi na hivyo kuathiri maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla ,lakini utapiamlo wa kuzidi au wa kupungua virutubishi mwilini unapelekea magonjwa ya mara kwa mara na magonjwa yasiyo ya kuambukiza na hivyo kuathiri kipato cha familia na sekta ya afya.

Aidha amesema,udumavu kwa watoto unasababisha madhara ya kiakili na kimwili ya muda mrefu yanayoweza kupelekea magonjwa ya mara kwa mara ,upungufu wa uelewa darasani hatimaye kuathiri uchumi wa nchi hapo baadaye .

“Tunaweza tukadharau suala hili la lishe tukawekeza kwenye barabara na vitu vingine ,lakini lazima tujue hivyo vikibomoka tunaweza kupata fursa ya kukarabati ,lakini kwenye lishe na ubongo wa mtoto ,hatuna fursa ya kukarabati  baada ya miaka mitano,kwa hiyo wakati wa kuwekeza kwa mtoto ni sasa na hapa tutapata Taifa lenye watu wenye tija.”amesema

Hata hivyo amesema,nchi inaenda vizuri katika suala la lishe huku akisema Tafiti za TDHS zinazotumika inaonyesha utapiamlo ,ukondefu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano  umepungua kutoka asilimia 4.5 mwaka 2015/16 hadi kufikia asilimia 3.5 mwaka 2018.

Kuhusu upungufu wa damu kwa wanawake wenye umri wa kuzaa umepungua kutoka asilimia 45 mwaka 2015/16 hadi asilimia 29 mwaka 2015/16 huku udumavu nao ukipungua kutoka asilimia 34 mwaka 2015/16 hadi kufikia asilimia 32 mwaka 2018/19.

“Lakini sasa hapa kwenye udumavu ,maana yake tunapozungumza asilimia 32,watoto wenye umri wa miaka mitano kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 ni kama takriban watoto milioni tisa kwa hiyo tunazungumza watoto milioni tatu Tanzania wana udumavu,wamedumaa na hawafundishiki,

 “Pia watoto hawa hawaelewi,hawawezi kuwa wabunifu katika kufanya kazi na kuleta maendeleo ya nchi ,tunaweza tukapishana huko mikoani,mawizarani lakini tayari ubongo wa huyo mwenzetu ulishadumaa hauwezi kubadilikahauwezi kuingiza vipya,hauwezi kuja na ubunifu wa mambo mapya.

Kutokana na hali hiyo amesema Wizara ya Afya itaendelea na jukumu la kuandaa na kuto sera miongozo na mikakati ya afya ikiwemo huduma za lishe na kuzifanyia kazi sera zilizopitwa na wakati kwa maslahi mapana ya watoto hapa nchini na Taifa kwa ujumla.

Kuhusu kupunguza udumavu kwa watoto amesema wataendelea kushirikiana na wadau wa lishe nchini kutekeleza afua za lishe zenye matokeo makubwa zinazolenga siku 1000 za maisha ya mtoto ikiwemo utoaji wa madini ya chuma na acid ya folic kwa akina mama wajawazito takriban kwa akina mama wajawazito milioni 2.3 kwa mwaka.

Naibu Katibu Mkuu Afya Dkt.Grace Maghembe amesema,mkakati uliowekwa ni kuwafikia wananchi ili waweze kuelewa suala hili la lishe kwa kurejesha siku ya maadhimisho ya lishe ya kijiji ili  iweze kuadhimishwa kwenye ngazi ya kijiji .

Vile vile amesema pia mpango ni kuelimisha jamii kupitia wahudumu wa ngazi ya afya ya jamii na kufanya vikao vya tathimini kwa ngazi ya kata na ngazi ya kijiji badala ya tathimini hizo kufanyika katika ngazi ya mikoa na halmashauri lakini pia kutumia mitandao ya kijamii ili elimu iweze kufika kwa jamii.

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.