Wadau wa Lishe wahimizwa kusaidia Lishe shuleni


NAIBU Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga wàkiwa wameshika fomu baada ya kutiliana Saini kuhusu Mpango wa Lishe shuleni na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Sarah Gordon-Gibson hafla iliyofanyika katika shule ya Mtemi Mazengo Ipagala Jijini Dodoma


NA JOYCE KASIKI,DODOMA

NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga amewataka wadau wa Lishe nchini kusaidia Mpango wa Lishe shuleni ili kuongeza mahudhurio shuleni utakaochangia ufaulu kuongezeka.

Kipanga ameyasema hayo jijini hapa katika  hafla ya kusaini fomu ya Muungano wa lishe shuleni baina ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na Shirika la Chakula Duniani (WFP).

Ameema mradi huo wa lishe ni muhimu sana mashuleni kutokana na kwamba unasaidia kuchochea mahudhurio ya wananfunzi,usikivu wa darasani lakini pia kuwajengea afya bora wanafunzi wanaohudhuria shuleni hapo. 


Kipanga amesema muungano huu Tanzania ni muhimu kwa sababu kutawezesha wadau wa maendeleo kuendelea kuhamasisha umuhimu wa chakula mashuleni.

Ameipongeza serikali kutokana na kukubaliana na suala la uwepo wa chakula shule kwa sababu unasaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea mahudhurio shuleni. 

Vile vile Kipanga amelipongeza  WFP kwa kuona umuhimu wa Lishe shuleni na  kuleta mradi huo .

Naye Mkurugenzi Mkazi wa WFP Sarah Gordon-Gibson ameishkuru serikali ya Tanzania kutokana na ushirikiano inaoonyesha katika kazi wanazofanya nao katika masuala ya lishe.

Godon amesema mpango wa chakula mashuleni ni mzuri sana kwa sababu unasaidia watoto kuelewa masomo yao vizuri kitendo kinachochangia kuongeza ufaulu darasani.

Mkurugenzi Mkaazi huyo wao kama WFP wataendelea kusisitiza nchi kujiunga katika mpango huo ambapo hadi sasa tayari nchi 52 zimeshaini fomu hiyo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Riziki Mdoe alisema suala la lishe mashuleni ni la muhimu sana hivyo WFP wamefanya jambo la muhimu kwa kusaini mkataba huo.

Kwa upande wa wanafunzi waliohudhiria hafla hiyo walitoa kumbe mbalimbali kupitia burudani ambapo walisema uwepo wa Lishe shuleni utasaidia kuongeza uelewa lakini pia utapungiza itoro shuleni na hivyo kuwezesha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.


Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.