Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
KUFUATIA vikundi vya uhalifu vikiwemo vikundi vya vijana wanaojiita panyaroad kuvamia nyumba za watu kufanya mauaji na kuiba mali,Serikali imeonya na kuwataka wahusika kuacha vitendo hivyo mara moja.
Akizungumza na wandishi wa habari leo Septemba 16 mwaka huu jijini Dodoma Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Ahmad Masauni amesema ipo mipango ya muda mfupi na muda mrefu katika kudhibiti hali hiyo ya uhalifu nchini huku akiwatoa hofu wananchi kwamba Serikali itamalimaza suala Hilo.
"Kumekuwa na matukio ya uhalifu ambayo yamewahi kutokea hapa nchini katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Mkuranga,Kibiti na Rufiji ,lakini vyombo vya usalama vilifanikiwa kudhibiti."amesema Mhandisi Masauni na kuongeza kuwa
"Katika Mpango wa muda mfupi wa kushughulikia na vikundi hivi vya uhalifu hakuna atakayebaki salama na walioshiriki kwa namna moja ama nyingine nao pia hakuna atakayebaki salama."
Mhandisi Masauni amesema,Mpango wa Jeshi la Polisi wa muda mrefu ni kushughulika na mtandao mzima unahisika katika vikundi hivyo wakiwemo wanaowasaidia kwa kununua bidhaa za wizi pamoja na wazazi wanaoshiriki kwa namna yoyote ile,nao hawatakuwa salama .
Hata hivyo kiongozi huyo amesema,wamebaini wanaoongoza mtandao wa vikundi hivyo vya uhalifu ni watu waliomaliza vifungo magerezani huku akisema tayari mikakati ya kushughulika nao imesharatibiwa .
Ameviasa vyombo vyote vya usalama vifanye Kazi kwa karibu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kushughulikia makundi hayo ya wahalifu.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillius Wambura ametoa pole wananchi waliokumbwa na kadhia yoyote ya vikundi hivyo vya uhalifu huku akisema tayari idadi kubwa ya wahalifu wamekamatwa na wanawndelea kuwakamata watu wote wanaoshiriki hata kwa kununua vitu vya wizi.
Amewaonya na kiwatahadharisha wahalifu ambao bado wanapanga kufanya uhalifu huo huku akisema vitendo hivyo havikubaliki na kwamba Jeshi la Polisi halitakubali lijirudie.
"Tunatoa tahadhari hii kwa vyombo vya habari ili wote wasikie au wenye ndugu zao wanaosikia waende kuwapa taarifa kwamba wakae chonjo ,huu ni wakati mbaya kwao ,Serikali kupitia Jeshi la Polisi haijawahi kushindwa kushughulika na wahalifu "amesema IGP Wambura
Pia ametumiwa nafasi hiyo kuwataka viongozi wa Serikali za Mitaa kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi ili vishirikiane na Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi.
No comments:
Post a Comment