KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Fatma Mganga akizungumza na wadau wa Maziwa nchini katika kongamano la wadau wa maziwa lililofanyika jijini Dodoma |
BAADHI ya wadau wa Maziwa |
WADAU wa Maziwa wakifautilia jambo kwenye kongamano la wadau wa maziwa lililofanyikaleo jijini Dodoma |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
KATIBU Tawala wa mkoa wa Dodoma Fatma Mganga
amewataka viongozi wa mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatafakari namna ya kuanza
kunywesha maziwa shuleni angalau kwa watoto wa darasa la awali hadi darasa la
nne ili waweze kupata lishe na kukua vizuri.
Mbali na hilo Halmashauri zinaweza kutumia fedha kiasi
cha shilingi 1000 kinachotengwa kwa ajili ya lishe shuleni kwa kila mtoto kwa ajili ya kununua maziwa na kuwapa
watoto ili waweze kuboresha afya zao badala ya kuzitumia katika masuala ambayo
hayana tija kwa afya za watoto hao.
Dkt.Mganga maeysema hayo leo jijini hapa wakati
akifungua kongamano la wadau wa maziwa ikiwa ni siku moja kabla ya kuadhimisha
siku ya unywajimaziwa shuleni.
Amesema inawezekana idadi ya wanafunzi wa shule
zote za msingi na sekondari wakawa wengi na hivyo kufanya mkoa kushindwa kumudu
gharama ya shughuli hiyo.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo malengo yatakayowekwa
na wadau wa kongaman hilo yatauhusu mkoa wa Dodoma ambao umekuwa ukikabiliwa na
changamoto ya udumavu ambayo huenda pia inasababishwa na watoto kukosa kunywa
maziwa.
“Malengo hayo
yatatufanya tukimbie ,na kwa mkoa wa Dodoma
mimi hayo malengo yatakuwa yananihusu sana,maana huwa tuna masuala ya lishe, hapa
tuna fedha ambazo halmashauri wanaambiwa watenge fedha za lishe angalau kila
mtoto shilingi 1000 ,
“Sasa nikawa nasema, kumbe hata hizi fedha kiasi
fulani tunaweza kukitumia kwa kununua maziwa wakanywa watoto shuleni kwa sababu
hiyo pia ni lishe ,lakini pia na sheria imeshatengenezwa kwamba shilingi 1000
hiyo isitumike kwenye masuala tu ya
kwenda kuangalia kitu fulani kuhusiana na masuala ya lishe ,au unakuta imetumika kwenye ‘supervision’
,kumbe ingetumika kununua maziwa watoto wangeboresha afya zao .”amesema na
kuongeza kuwa
“Hata kama shule hatuwezi kunywesha watoto wote
basi inyweshe kuanzia angalau chekechea’darasa la awali’ hadi darasa la tatu ,au
la nne ,kwa mfano hapa Dodoma tuna
watoto kama laki tisa hivi ..,watoto wa sekondarti
kama laki tatu na laki sita ni shule za msingi,lakini
tukiangalia inawezekana laki sita ukawa mzigo mkubwa sasa labda tuchukue darasa
la awali hadi darasa la tatu au la nne
ambao wapo kwenye umri wa kuendelea kukua, amesema na kuongeza kuwa
“Hivi unaweza kufikiria mtoto wa chekechea kinatakiwa
kiwahi mwisho wasiku mtoto anakuja shule ana njaa,hakuna uji wala chakula
chochote ,mtoto anaanza kuchukia shule tangu akiwa darasa la awali ,sasa ili
watoto hawa wadogo waweze kupenda shule na kusoma ni kaunzisha miakati ya
kunywa maziwa hasa kwa watoto wadogo wa darasa la awali mpaka darasa la nne.”amesema
na kuongeza kuwa
“Tunaposema udumavu, ni ukuaji wa mtoto unakua umeathirika
sasa tukishakuwa na watu ambao hawakui vizuri sijui hilo linakwenda kuwa ni
Taifa la aina gani maana yake ukuaji ni pamoja na ukuaji wa ubongo kama ubongo haujaukua vizuri huyu mtu atakuwa
na mikakati kweli yakuendeleza nchi ,anaweza kuwa na mikakati ya kuboresha
uchumi?,haiwezekani sasa haya mambo ni ya msingi sana na tusilichukulie kama
suala la kawaida.
Ameomba kongamano litoke na mikakati ambayo ndiyo
itakuwa faida kwa wadau hao kufanya kongamano katika mkoa wa Dodoma na sisi
watendaji tupate kitu cha kusmmamia na kuonyesha katika kongamano la mwaka
ujao,tunaweza kualikwa tukatoa taarifa kwamba tumefanya hivi na hapo ndipo
dhamira ya kweli itakapotimia .
Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa Nchini Zacharia
Masanjiwa amesema,bado kuna changamto ya unywaji maziwa hapa nchini huku
akisema,licha yakuwa Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na mifugo mingi katika
Bara la Afrika lakini bado kuna changamoto ya unywaji maziwa ambapo mtu mmoja
hunywa maziwa lita 62 badala ya lita 200 kwa mwaka.
“Lakini hata hivyo kwatakwimu hizo inawezekana
wanaokunywa maziwa mengi ni watu wazima sasa tunataka tulenge kwa watoto katika
kuhakikisha wanakunywa maziwa shuleni.”
Kwa upande wake Msajii wa Bodi ya Maziwa nchini
George Msalya amesema,wadau lazima sasa waanze kutekeleza suala la unywaji
maziwa shuleni kwa vitendo na siyo kuendelea kufanya kwa mazoea.
No comments:
Post a Comment