Waziri wa Maji Jumaa Aweso
NA MWANDISHI WETU ,DODOMA
BUNGE limepitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2022 (The Water Resources Management Act, 2022).
Muswada huo umepitishwa
leo 15 Agosti, 2022 ambapo kupitishwa kwa sheria hiyo kutaimarisha Bodi za mabonde ya Maji katika kusimamia Rasilimali za Maji nchini vilevile kuimarisha uhifadhi wa Vyanzo vya Maji nchini ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa Maji majumbani na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Wabunge waliochangia Muswada huo wamempongeza Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwa kutambua umuhimu wa utunzaji, uhifadhi na uendelezaji wa Rasilimali za Maji wakieleza kwamba Muswada huu umekuja wakati sahihi ambapo kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya Maji ikiwa kiwango cha Rasilimali za Maji kiko palepale.
Awali akiwasilisha muswada huo,Waziri Aweso ameahidi mbele ya Bunge kuendelea kutoa elimu na ushirikwaji kwa wananchi kuhusu utunzaji na uhifadhi wa Rasilimali wakati akijibu hoja mbalimbali.
Aidha ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wabunge kwa kuunga mkono muswada huo kwa asilimia mia na kuahidi kuzingatia maoni, mapendekezo na ushauri wao katika Utekelezaji wa Sheria mbalimbali zinazohusiana na uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya Maji.
No comments:
Post a Comment