RAIS Samia Suluhu Hassan |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
RAIS Samia Suluhu Hassan ameiagiza Mawakili wa Serikali kushughulikia
kwa haraka na haki kesi za uwekezaji kwa
lengo la kukuza uchumi wa nchi huku akipiga marufuku kusainiwa mikataba ya
Serikali bila kushirikisha ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) .
Akizungumza leo Septemba 29 ,2022 mwaka huu jijini Dodoma kwenye Mkutano
wa Chama cha Mawakili wa Serikali Rais Samia amesema,kwa kuishirikisha ofisi ya
AG katika kusaini mikataba hiyo itakwenda kuleta maslahi mapana kwa wananchi na
Taifa kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Rais Samia ,huko nyuma mikataba ilisainiwa bila ofisi ya
AG kujua na wanapopata tatizo ndio
wanaikumbuka ofisi hiyo na huenda wakati huo waliosaini wameshastaafu au
wamtangulia mbele ya haki.
“Ninyi ndiyo majeshi ya kulinda
uchumi wetu kisheria ,uwekezaji lazima ulindwe lakini pia biashara lazima
zilindwe,na watu kulinda hayo yote ni ninyi,ninyi ni walinzi wa kalamu na
sheria siyo walinzi wa mabunduki kwa hiyo mwende mkalinde uchumi wetu ili nchi
hii iweze kupokea wawekezaji wengi zaidi, tuwekeze na tukuze uchumi kwa maslahi
mapana ya Taifa.”amesema Rais Samia
Kwa upande wake Waziri wa Katiba
na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amesema wizara inaanzisha mpango mahususi wa
utoaji msaada wa kisheria ambao utaluwa endelevu kwa lengo la kuwasaidia
wananchi ambao hawezi kumudu gharama.
Aidha amesema mpango huo utazinduliwa Desemba 10 mwaka huu ambapo siku hiyo , ni
siku ya haki duniani .
No comments:
Post a Comment