Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Bia la Taifa (NIC) Karimu Meshack akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa chama cha Mawakili Tanzania |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
MKUU wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Bima la
Taifa (NIC) Karimu Meshack amesema,Shirika hilo ni moja ya mashirika bora
yanayotoa huduma bora za bima kwa wananchi zinazohusiana na majanga mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati
wa Mkutano wa Chama cha Mawakili Tanzania,Meshack amesema,lengo la shirika hilo
ni kutoa huduma bora kwa watanzania waliojiunga na shirika hilo kwa wakati
pindi wanapopata majanga mbalimbali.
“NIC ni Shirika la serikali lakini pia ni shirika
la kibiashara la kutoa huduma za Bima za mali na ajali pamoja na bima za maisha
,shirika mwanzo lilikuwa haliwezi kutengeza faida hivyo lilikuwa likijiendesha
kwa hasara,lakini kwa miaka minne mfululizo limekuwa likiendeshwa kwa faida
ambapo kwa mfano rekodi ya mwaka 2020/21 tumeweza kutengeza faida ya shilingi
bilioni 72.”amesema Meshack
Amesema Shirika hilo limeweza kutengeza faida
kutokana na mapinduzi ya kimaendeleo katika maeneo matatu ikiwemo eneo la
rasimaliwatu kwa kutafuta wataalam wenye weledi wa kuweza kuliendesha shirika
pamoja na vijana wenye uwezo wa kufanya biashara
“Pia katika eneo la kimifumo ambapo shirika
linaendeshwa kidigitali shughuli zote za kibima zinafanyika kwenye sytems na
tumeanzisha mfumo ambao unatuwezesha kutoa huduma kwa wateja kwa haraka na
ufanisi wa kiwango cha juu,
“Kwa mfano katika shirika letu ndani ya siku saba
mteja anakuwa ameshapata huduma,ndani ya saa 24 mteja anapokuja kukata bima
anatakiwa kuwa ameshahudumiwa na anaendelea na shughuli zake kama kawaida.
Aidha amesema hivi sasa NIC lipo kwenye maeneo yote
nchini lakini kwa sababu ya maendeleo ya sayansi na teknolojia iliyopo mteja
anaweza kupata huduma za kibima kwa kutumia NIC Kiganjani akiwa mahali popote ili
mradi mteja awe na pesa kwenye simu yake ya kiganjani.
“Eneo lingine ni la kiubunifu , sasa hivi tume-‘restructure’
(tumetengeneza upya) bidhaa zetu zote za
kibima kwa mfano tunasukuma bidhaa moja ya Bimlife ambayo biashara hii
imefanyiwa utafiti kwa ajili ya kwenda kujibu changamoto zinazomkumba mtanzania
wa kawaida,
“Mfano hii Bimlife inatoa mafao ya msiba kwa
mwanachama aliyepatwa na msiba ambapo haina maana kwamba fedha ya rambirambi ,na
kwa kupata kwako fidia ya rambirambi haina maana kwamba itaenda kuchukua fedha
ulizowekeza kwenye Bimlife,ukifika wakati wa kupata mafao yako unayapata kwa
kiwago kile kile kwa mujibu wa mkataba lakini wakati huo masuala ya fidia au
rambirambi yanakuwa kama bonus .
Meshack ametumia nafasi hiyo kuwaasa watanzania
wajiunge na NIC ili waweze kupata huduma
za bima kwa sababu ni shirika ambalo linalipa ,na linaloongoza kwa mtaji ndio maana
‘tunasema sisi ndio Bima wengine wanafuata’
Kwa mujibu
wa Meshack Shirika lipo kwa ajili ya kusapoti jitihada za Serikali ya Jamhuri
ya Muungano ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwapasapot
kwenye miradi ya kimaendeleo,kuwapa sapoti kwenye shughuli za kiserikali na
watanzania wote kwa kurudisha kile kinachopatikana kwenye jamii.
“Kwa hiyo tunawashauri waje wakate bima
mbalimbali,kwa mfano bima ya nyumba ,watu wanafikiri kuna thamani kubwa sana
kukata bima ,nyumba ya milioni 100 ukiikatia bima NIC unalipia shilingi 177,000
kwa mwaka ,kwa hiyo upote nyumba yako ya milioni 100 uliyoisumbukia kwa miaka
mingi kuijenga ndani ya dakika moja,ndio maana tunawakaribisha watanzania waje
walitumie hili ni shirika lao.”amesisitiza
No comments:
Post a Comment