KATIBU wa Halamshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka |
Wajumbe wa Halamshauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) jijini Dodoma ukumbi wa White House wakiwa katika kikao cha uteuzi wa wagombea ngazi ya wilaya |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ,Itikadi
na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa watu zaidi ya milioni mbili
wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho kuanzia
ngazi ya mashina hadi Taifa.
Aidha Shaka amesema kuwa chama hicho kimeongeza
muda wa kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi ya Halamshauri Kuu ya CCM
Taifa (NEC) huku kionya wanaokiuka taratibu za chama hicho.
Akizungumza mara baada ya kuhitimishwa kwa vikao
vya juu vya chama hicho chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Samia Suluhu Hassan jijini
Dodoma vilivyoketi kwa ajili ya kufanya teuzi za wagombea wa nafasi za ngazi ya
wilaya Shaka amesema,kwa watakaokiuka taratibu hatua zitakazochukuliwa ni
pamoja na kufuta chaguzi husika.
“Kamati Kuu ya CCM Taifa imeongeza muda wa kuchukua
na kurejesha kwa hiyo kuanzia tarehe moja hadi tarehe tatu,zoezi la kuchukua na
kurejesha fomu kwa ngazi za mikoa na Taifa zoezi hilo litafanyika ,
“Kufunguliwa kwa dirisha hilo tutapata viongozi
wengi zaidi ambao wanaingia kwenye ushindani hatimaye tuwekuwapata wale
watakaowakilisha ngazi ya Taifa na ngazi ya mkoa.”amesema na kuongeza kuwa
“Eneo moja tutakalosimamia kwa nguvu zote ni eneo
la matumizi mabaya ya madaraka kwa maana kwamba kutumia rushwa ili kuweza
kupata madaraka ya uongozi ,hii ni kuhakikisha tunapata viongozi bora na siyo
bora viongozi.”
Aidha amesema hatua ya wanachaa zaidi ya milioni
mbili kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho inaonyesha jinsi ambavyo
chama hicho kina watu wengi na wenye sifa za uongozi.
Shaka amesema,Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja
na mambo mengine imefanya uteuzi wa mwisho wa nafasi za wagombea wangazi za
wilaya nchi nzima.
“Kwa hiyo tumeteua na tumeshapata wagombea ambao
watakwenda kusimama kwenye uchaguzi wa ngazi ya wilaya ambao utafanyika Oktoba
Mosi na mbili mwaka huu nchi nzima”amesema Shaka
Amewataka wanachama wote wenye sifa ya kushiriki kuwachagua viongozi hao wa wilaya wajitokeze kwa wingi katika maeneo yao katika tarehe hizo kwa mujibu wa ratiba ambazo zitapangwa na mkoa na ngazi ya wilaya.
No comments:
Post a Comment