MKURUGENZI wa Mtandao wa Malezi na Makuzi ya Watoto ( TECDEN) akiwa katika hafla ya uzinduzi wa PJT-MMMAM ngazi ya mkoa (mkoa wa Dodoma) |
MKURUGENZI wa Shirika liliso la Kiserikali Action for Community Care (ACC) linalotekeleza mradi wa toto Kwanza Pendo Maiseli |
BAADHI ya wadau wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) mkoa wa Dodoma. |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
MKURUGENZI wa Mtandao wa Malezi na Makuzi ya Watoto
nchini (TECDEN) Mwajuma Rwebangila amewaasa wadau wa mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali wenye malengo ya watoto washirikiane na Serikali kuhakikisha
Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) itakayowezesha watoto kulelewa na
kufikia utimilifu wao.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
uzinduzi wa Programu hiyo kwa ngazi ya mkoa,Mkurugenzi huyo amesema,wadau wana kila sabahu ya kuelimisha jamii umuhimu
wa kuwekeza kwa watoto wadogo .
“Kuwekeza kwa watoto wadogo ni muhimu
sana,inawezekana Taifa tunalolieona sasa hivi lina mwanzo wake ,na tunaamini
kwamba ukibadilisha mwanzo wa hadithi ,umebadilisha hadithi nzima,
“Kwa hiyo tubadilishe mwanzo wa hadithi toka mimba
inatungwa mtoto alelewe katika kuhakikisha anakuwa na afya bora,lishe ya
kutosha,ulinzi na usalama wa mtoto,Malezi yenye mwitikio na fursa za ujifunzaji
wa awali.”amesema Rwebangila na kuongeza kuwa
“Watoto wapewe fursa za kucheza ,na kwa kucheza mtoto
anajifunza vitu mbalimbali,anaweza kutengeneza kitu na ukimwambia akuelezee
atafanya hivyo,hiyo inatosha kufanya akili na ubongo wake kufanya kazi kwa
haraka.”
Kwa mujibu wa Rwebangila TECDEN wanashirikiana na Umoja wa Klabu za
waandishi wa habari nchini (UTPC) kupitia Shirika lisilo la kiserikali
linaoshughulika na masuala ya Malezi na Makuzi ya Watoto (CiC) linalotekeleza
mradi wa miaka mitatu wa Mtoto kwanza.
Rwebangila amesema,mradi huo umelenga kuchochea utekelezaji
wa PJT-MMMAM katika kuhamasisha sekretarieti za mikoa kuhakikisha Programu hiyo
kubwa ya Taifa inafahamika na itekelezwa katika ngazi za Mikoa na Halmashauri.
Naye Meneja Programu Mradi wa Mtoto kwanza unatekelezwa
mkoani Dodoma na Shirika lisilo la
Kiserikali la Action For Community Care (ACC) Magret Mukama amesema,mradi huo
umejikita kusaidia watoto walio na umri wa miaka 0-8 ili kuharakisha
upatikanaji wa matokeo chanya ya Maendeleo ya Awali ya Mtoto katika utoaji wa
huduma za malezi jumuishi .
“Maana
wataalam wanasema katika kipindi hicho mtoto ubongo wa mtoto unakua kwa kasi na mtoto anakuwa na
uwezo wa kujifunza na kuelewa kwa haraka ,ndiyo maana mradi umejikita katika
kusaidia kundi la watoto hao kwa ajili kuwa na Taifa lenye tija kwa Taifa hapo
baadaye.”alisema Mukama
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya
Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum Salome Francis amesema, mpaka sasa Programu imeziduliwa kwenye Mikoa tisa
ya Tabora, Morogoro,Lindi, Arusha,
Manyara, Mbeya, Rukwa, Kagera na Dar Es Salaam huku Dodoma ukiwa mkoa wa 10
Kuzindua programu hiyo.
Aidha amesema, baada ya
uzinduzi huo wataalam kutoka kada mablimbali za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa
Jamii, Afya, Lishe, Elimu, na Mipango Pamoja na Asasi za Kiraia kutoka
Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma watajengewa
uelewa kuhusu PJT-MMMAM na baadae kuandaa mpango kazi wa utekelezaji wa kipindi
cha mwaka mmoja kwa kila Wilaya ambao utasaidia katika kupima utekelezaji wa
Programu.
No comments:
Post a Comment