Wamachinga jiji la Dodoma waanza kuhamishiwa kwenye soko jipya,Jiji kukusanya sh.1 bil kwa mwaka

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Joseph Mafuru (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini humo.



NA JOYCE KASIKI,DODOMA

MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema soko la Wamachinga lililojengwa katika eneo la Bahi Road jijini humo limekamilika huku akisema matarajio yao ni kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.2  kwa mwaka ambapo tayari shughuli ya kuwapeleka wamachinga katika soko hilo imeshaanza.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema,kutokana na wamachinga kuendelea kujitokeza kila siku,Jiji la Dodoma limepanga kuendelea kujenga masoko kama hayo katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini humo,Mafuru alisema shughuli ya kuwahamisha wamachinga tayari imeshaanza huku septemba 23 mwaka huu ndio itakuwa mwisho wa wamachinga kuonekana wakifanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi.

"Kuanzia Leo Watu wanaanza kuingia kwenye soko la wamachinga,kwa hiyo kuanzia Septemba 24 mwaka huu hatutamwona Machinga yeyote nje ya soko lile. “alisema MafuruDodoma manunuzi yote Watu wajue yatafanyika kwenye soko la wamachinga " alisema Mafuru

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo,uwezo wa soko hilo ni kuchukua wamachinga 5000,lakini mpaka sasa uhakiki unaonyesha wapo wamachinga 3000,maana yake waliopo mtaani wanaondoka wote hakuna atakayebaki nawatakapokuja wapya tutawajazia pale kwa kuzingatia wale tu wenye sifa za kuingia pale.”alisisitizana kuongeza kuwa

“Kwa hiyo yeyote hata kama ndio unaanza leo utaingia kwenye soko na hata kama utakosa pale utaingia kwenye masoko tuliyoyaandaa ila utaratibu ni kwamba kwa wale tuliowasajili mwanzo watatangulia ,na wale wanaoongezeka tutaendelea kuwapokea.’

Hata hivyo alisema mpaka sasa hatujapata malalamiko ya watu ambao hawajahakikiwa na zoezi la uhakiki halijawahi kufungwa huku akisema,hata sasa bado wanaendelea kuwapokea na kuwahakiki kwa lengo la kupata nafasi.

“Lakini tunajua hii ni ajira ,sasa kwa wale watakaoongezeka  watenda kwenye ‘D  centers’  zetu,wengine wanaoendelea kuongezeka jiji litajenga masoko mengine ya wamachinga eneo la Nzuguni pamoja Mnadani.

Amesema,makusanyo yatakayotokana na soko hilo yatatumika kujenga masoko mengine yenye mfano wa soko hilo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma ambayo wamachinga wataendelea kuwekwa na kufanya biashara kwenye masoko hayo.

Kufuatia kukamilika kwa soko hilo amesema,hatarajii kuona mfanyabiashara anafanya shughuli zake katika maeneo yasiyo rasmi na kwamba wafanyabiashara wote wanapaswa kwenda kufanya biahsra katika soko hilo ambalo limejengwa kwa ajili yao.

Mafuru amesema,kuanzia tarehe hiyo,manunuzi yote yatakuwa yanafanyika katika soko la Wamachinga na siyo kwenye mitaa kama ilivyozoeleka .

“Ujenzi wa Soko  umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 9.53 mpaka kukamilika kwake ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alitoa shilingi bilioni 3 na sisi kama Jiji tulitoa kiasi cha shilingi bilioni 6.5 Kwa kutumia mapato ya ndani kuongeza na kufikia kiasi hicho kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa soko hilo.”alisema Mafuru

Amesema , katika soko hilo kumewekwa  mfumo wa kisasa kwa ajili ya Wafanyabiashara hao wadogo wadogo ambapo kwa sasa wameanza kufanya uhakiki ili kupata watu waliolengwa kufanya biashara katika soko hilo.

Vile vile amesema,zimefungwa kamera za kisasa za kudhibiti wizi huku akisema katika soko hilo hakutakuwa na wizi kwani kila atakayefanya uhalifu wowote atabainika mara moja.

Mkurugenzi huyo amesema,kukamilika kwa soko hilo kunakwenda kulifanya jiji la Dodoma kuwa safi.

" Tuligundua hata viongozi wa juu Wafanyabiashara ndogo ndogo Kwa namna Moja ama nyingine walifanya mji uonekane haupendezi . "

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.