Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Katumba (2)Mauyeni kilumbe |
SERIKALI kwa kushirikiana na wadau wameombwa kuchangia upatikanaji wa vifaa ikiwemo baiskeli kwa watoto wenye ulemavu wa viungo na uoni hafifu katika shule msingi mchanganyiko ya Katumba (2)iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya .
Akizungumza na Habarinews Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Katumba (2)Mauyeni kilumbe amesema kuwa shule hiyo ina uhaba wa vifaa saidizi kwa watoto wenye ulemavu kutokana na wengine kutambaa kutokana na ukosefu wa baiskeli.
Kilumbe ameomba wadau kutoa misaada mbali mbali na kusema vifaa vilivyopo havitosherezi mahitaji ya watoto wenye ulemavu , wengine wanatumia mashine za kuandikia za nukta nundu , wenye uarubino wanauhitaqji wa mafuta ,kofia na mahitaji mengine muhimu .
“Kwasasa hivi tuna baiskeli tano tu ambazo nazo hazitosherezi maana hapa tuna watoto wengine hawawezi kutembea bila baiskeli na `zilizopo zina uchakavu kilichopo hivi sasa tuna uhitaji wa baskeli 16 kwa watoto wenye ulemavu wasiojiweza kabisa,ila mahitaji zaidi ni baskeli 16, na mashine 24 za kuandikia za nukta nundu kwa wenye uoni hafifu , "amesema
Aliongeza kuwa "watoto watano wanatumia vibao vya kawaida hizi mashine mpya tunazofatilia tunaambiwa zimepitwa na wakati lakini kwa mpya kabisa za kisasa ni shilingi mil.1 hivyo tunaomba wadau na jamii kujitokeza kusaidia watoto hawa “amesema Mkuu huyo wa shule .
Aidha aliomba wazazi kuzidisha upendo kwa watoto wao wenye ulemavu kwa kuwaleta shule kwani shule hiyo haina malipo yoyote na kusema kuwa kitendo cha kumficha mtoto mwenye ulemavu ndeani ni kumnyima haki ya kupata elimu .
Akizungumzia kuhusu wadau ambao wamekuwa wakisaidia shule hiyo Kilumbe amesema Child Support Tanzania kwa jitihada zake za kuhakikisha kuwa kusaidia wanafunzi wenye ulemavu kwa kutoa vifaa saidizi pamoja na elimu na kuhamasisha wazazi wanaoficha watoto majumbani kuwapeleka shule.
Kwa upande wake Ofisa elimu Msingi halmashauri ya Busokelo ,Atuvonwe Chaula amesema kuwa kwa halmashauri hiyo wamekuwa wakifanya jitihada za kuwatumia walimu maalum kwenda vijijini kuwatambua watoto walemavu baada ya wazazi kutambua kuwa watoto wao walikuwa wanaachwa.
Damas Mwambeja ni Mwakilishi wa watu wenye ulemavu aliwataka wadau kuendelea kusaidia shule ya Katumba (2)na kusema licha ya serikali kuwa mstari wa mbele kusaidia shule hiyo basin a wadau na jamii wana wajibu wa kusaidia vifaa mbali mbali .
No comments:
Post a Comment