Bajeti ya TAMISEMI yapita kwa kishindo

Waziri Innocent Bashungwa


 

JOYCE KASIKI,DODOMA

BUNGE limepitisha kiasi cha shilingi trilioni 8.779 ikiwa ni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 kwa ajili ya Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) .

Awali akijibu hoja za wabunge waliochangia bajeti hiyo,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI Innocent Bashungwa alitumia fursa hiyo kuwaomba wabunge waipitishe bajeti ya ofisi hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka ujao wa fedha zikiwemo hoja zao zilizobaini mapungufu mbalimbali.

 

Ununuzi wa Pikipiki 68 za Maafisa Ustawi wa Jamii

Katika eneo hilo Bashungwa alitoa ufafanuzi ambao alisema ulisababishwa na makosa ya kiuandishi ambapo amesema,ununuiz wa pikipiki hizo uligharimu shilingi milioni 227.50  ambazo zilitolewa na wadau tofauti na alivyosema katika hotuba yake April 14 mwaka huu kwamba pikipiki hizo zil;inunuliwa kwa gharama ya shilingi milioni 789.9 .

 

 “April 14 mwaka huu  niliwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais–TAMISEMI kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2022/23,katika eneo la utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi Rais-TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2021/22, sehemu ya Huduma za Ustawi wa Jamii nilisoma kwamba, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imefanya ununuzi wa Pikipiki 68 aina ya “boxer” zenye thamani ya Shilingi milioni 789.9 kwa ajili ya Maafisa Ustawi wa Jamii’.”amesema na kuongeza kuwa

 

Ninaomba kutoa taarifa kwamba, idadi ya pikipiki 68 iliyotajwa kwenye hotuba yangu siyo sahihi na hii imetokana na makosa ya kiuandishi,usahihi ni kwamba pikipiki 68 zimenunuliwa na wadau kwa gharama ya Shilingi milioni 227.50 ambao walikuwa wanatekeleza miradi ya “USAID Kizazi Kipya” katika baadhi ya Halmashauri katika Mikoa 21 ambazo zilinunuliwa na kusambazwa mwezi Septemba, 2021.”

 

Bashungwa amesema, kwa lengo la kutosheleza mahitaji ya pikipiki kwa Maafisa Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais-TAMISEMI iliona inunue pikipiki 200 aina ya “boxer”, ambazo kwasasa ziko katika hatua ya mwisho ya manunuzi na kwamba  Pikipiki hizi zinanunuliwa kupitia fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO -19 kwa gharama ya Shilingi milioni 562.40.

 

Pikipiki hizo zitasambazwa kwenye maeneo ambayo hayakupata mgao wa pikipiki 68. Hivyo, jumla ya Pikipiki 268 zitanunuliwa kwa gharama ya Shilingi milioni 789.90. Aidha, taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba OR-TAMISEMI imenunua pikipiki moja kwa Shilingi milioni 11 siyo sahihi. Taarifa sahihi ni kwamba kila pikipiki kati ya pikipiki 68 ilinunuliwa na mdau wa maendeleo kwa Shilingi milioni 3.34.

 

Miundombinu ya Wafanyabishara Wadogo (Machinga)

Amesema katika kuboresha miundombinu ya kufanyia biashara kwa wafanyabiashara wadogo (machinga), Serikali imechukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha shughuli zao zinafanyika kwa tija huku akisema ujezni wa soko la Machinga Dodoma lililojengwa kwa fedha za ndani za mapato ya Jiji la Dodoma linapaswa kuwa soko la mfano lilopaswa kujengwa katika miji na majiji.

 

Kwa mujibu wa Bashungwa ,hatua ambazo zimechukuliwa ni pamoja na kuwapanga Machinga kwenye maeneo rasmi kwa utulivu pasipo kutumia nguvu katika Halmashauri zote zilizokuwa na machinga wengi kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa. Hatua nyingine iliyochukuliwa ni Serikali kutoa 0 Shilingi bilioni 5.0 kwa ajili ya kuboresha maeneo ya kufanyia biashara machinga katika Halmashauri 11.

 

Amesema hatua nyingine inayoendelea ni kuwepo kwa majadiliano na Wizara ya Fedha na Mipango ili kufanya marekebisho ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290 ili kuruhusu sehemu ya fedha za Mikopo ya asilimia 10 kutumika katika kuboresha miundombinu ya Machinga ambapo  Marekebisho ya Sheria hiyo yanapendekezwa kufanyika kupitia Sheria ya Fedha ya Mwaka 2022. Majadiliano hayo yakikamilika, tunatarajia kiasi cha Shilingi bilioni 38.01 zitapatikana kupitia mlango huo kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya Wafanyabiashara Wadogo (Machinga).

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)

Akijibu hoja za wabunge kuhusu suala la TARURA Waziri huyo amesema   baada ya bajeti kupita ,katika mwaka wa fedha 2022/23, ununuzi wa kazi utaanza mwanzoni mwa mwezi Mei, 2022 ambapo amesema utaratibu huo umetokana na mapendekezo ya Kamati ya USEMI pamoja na Wabunge.

“Ninaagiza Mameneja wa TARURA wa Mikoa na Wilaya wawashirikishe Wadau ikiwa ni pamoja na Wabunge wakati wa kuainisha vipaumbele,na ili kuboresha ugawaji wa rasilimali fedha TARURA inafanya mapitio ya formula itakayotumika katika kugawa rasilimali fedha za ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara kulingana na hali ya maeneo husika.”

 

 Ufuatiliaji na Tathmini (Uratibu katika ngazi ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mikoa na Halmashauri)

Katika eneo hilo Bashungwa amesema,Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeimarisha mfumo wa kupima utendaji wa Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kwa kutumia viashiria muhimu (KPI) vikiwemo ukusanyaji wa mapato ya ndani, upelekaji wa fedha kwenye miradi ya maendeleo, matumizi sahihi, usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 ikiwa ni pamoja na marejesho, usimamizi wa miradi ya maendeleo na uzuiaji na utekelezaji wa hoja za ukaguzi.

Matokeo  ya upimaji yatatoa tafsiri ya utendaji wa Viongozi wengine katika ngazi ya Mkoa na Wilaya ambao wana jukumu la kuhakikisha kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatimiza majukumu yao.”amesisitiza

 

“ Hivyo, nitoe rai kwa Viongozi wote katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutimiza wajibu wao kwa kuwa utendaji wao utapimwa kwa kutumia viashiria hivyo..,Miradi ya Afya na Elimu nje ya ile ya UVIKO-19 ikamilike ifikapo tarehe 30 Mei, 2022 na hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Mikoa simamieni hii ‘deadline’.”

 

Ujenzi wa Vituo vya Afya vya Tarafa na Kata za Kimkakati

Kuhusu ujenzi wa vituo vya Afya Waziri huyo amesema,Ofisi ya Rais -TAMISEMI inatambua umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika uendelezaji wa miundombinu sambamba na kuiwezesha kutoa huduma za afya kwa kuwa na Vifaa Tiba na watumishi ambapo katika kutekeleza hilo imeweza kufanya tathmini ya uhitaji wa vituo vya afya 428 ambavyo vitajengwa kwa kipindi cha miaka mitatu  ijayo kuanzia Mwaka wa Fedha 2023/24.

Amesema vituo hivyo vitajengwa katika Tarafa zisizokuwa na Vituo vya Afya na Kata za kimkakati huku akisema kuwa katika mwaka wa Fedha 2022/23 Serikali itatafuta fedha kutoka kwa wadau mbalimbali, bajeti ya Serikali na Halmashauri kutumia Mapato ya Ndani.

 

xxxxxxxx

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.