Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) Charles akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu ukaguzi uliofanywa na ofisi yake kwa mwaka ulioishia Juni 30,2020/2021.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya CAG wakimsikiliza
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
JOYCE
KASIKI,DODOMA
UKAGUZI
uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Serikali (CAG) Charles
Kichere katika mwaka ulioishia Juni
30,2020/2021,umebaini mapungufu katika Mfuko wa Bima ya Afya yaliyoonyesha
madai ya Bima ya Afya yanaonesha madai ya wanaume 56 walipata huduma ya
upasuaji au za kawaida za kujifungua wakati huduma hizo zinatolewa kwa
wanawake.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dodoma April 12 mwaka huu wakati
akiwasilisha ripoti yake ya mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2020 /2021 CAG
Kichere amesema kuwa pia wanachama 444 walipata huduma ya kuchunguzwa picha
kamili ya damu ( full blood picture), zaidi ya mara moja kwa siku hadi mara 30
kwenye kituo kimoja.
Aidha
amesema ,kuwapo kwa malipo ya madai yaliyorudiwa pamoja na madai yanayoonesha
wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), walipokea miwani ya
kusomea zaidi ya mara moja wakati utaratibu unaruhusu kutoa miwani mara moja
kwa mwaka.
“Udhaifu
huo umesababishwa na kukosekana kwa udhibiti katika mfumo wa madai
iliyosababisha hasara ya shilingi milioni 14.41 katika mfuko.”amesema Kichere
na kuongeza kuwa
"
Ninapendekeza Mfuko wa Bima ya Afya kurejesha kiasi kilichopotea kutoka kwa
watoa huduma za afya husika,kuboresha mfuko wa madai wa CMIS ili kuhakikisha
unasaidia maafisa wanaohusika kuangalia uhalali wa madai yaliyowasilishwa”
Aidha Kichere
amesema kuwa ukaguzi huo pia ulibaini miamala 17 yenye jumla ya Lita Milioni
31.12 za mafuta zenye makadirio ya ushuru wa forodha shilingi Bilioni 2.89
ambayo hayakuainishwa kama ni kwa matumizi ya ndani au kusafirishwa kwenda Nchi
jirani huku akisema kuwa hiyo inaashiria kwamba mafuta hayo yalitumika nchini na yalipaswa
kutozwa ushuru wa forodha shilingi Bilioni 2.89.
"Ninapendekeza
kwamba Serikali iimarishe mifumo ya Udhibiti na usimamizi wa mafuta yanayoingia
nchini ili kuzuia matumizi ya mafuta hayo nchini bila Kodi stahiki kulipwa,Mafuta yaliyopitiliza
muda wa kukaa nchini ambayo yalipaswa kwenda Nchi jirani yenye ushuru wa
forodha shilingi Bilioni 1.78,"alisema. Kwa mujibu wa CAG Kichere Lita 2.63 za mafuta zenye makadirio ya Kodi ya shilingi Bilioni
1.78 ziliingizwa nchini kwaajili ya kusafirishwa kwenda Nchi jirani,hata hivyo
mafuta hayo hayakusafirishwa kwenda Nchi husika kwa zaidi ya miezi 12 kinyume
na Sheria ya forodha inayotaka yasafirishwe ndani ya siku 30. Akitoa mapendekezo ya ofisi yake kuhusu ripoti hiyo ameishauri Serikali iimarishe mifumo ya Udhibiti na usimamizi wa mafuta hayo nchini
bila Kodi stahiki kulipwa,pia mamlaka ikusanye ushuru wa forodha wa shilingi
Bilioni 1.78 kwenye Lita Milioni 2.63 pamoja na adhabu kwa mafuta ambayo
hayakuondoshwa nchini.
|
No comments:
Post a Comment