TPDC yaeleza ilivyojipanga kufikisha huduma ya gas asilia kwa wananchi

 

Afisa Usalama Mahala pa Kazi Deusdedit Kiheka akiwa katika banda la Shirika la Petroli nchini jijini Dodoma akionyesha namna ya kuvaa mtungi wa oksijeni mtu anapokuwa  kwenye moshi au mahali ambapo hakuna hewa ya oksijeni ya kutosha (SCBA).

 

JOYCE KASIKI,DODOMA

SHIRIKA  la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) limesema,linaendelea kufanya taratibu za kuwaunganisha wananchi na gas asilia inayosafirihswa kwa bomba la mafuta lilijengwa kutoka Dar es Salaam hadi Mtwara kwa ajili ya matumizi ya majumbani ambapo kwa mkoa wa Lindi pekee tayari wateja wapatao 200 wameshaunganishwa .

Akizungumza jijini hapa kwenye maonyesho ya Usalama na afya mahala pa kazi yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA) na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Afisa Maendeleo ya Jamii,Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano  wa TPDC Jackob Haule amesema  kazi hiyo inafanywa na TPDC kwa kushirikiana na kampuni yake Tanzu ya Gasco .

Amesema,mradi huo wa kusambaza gas asilia kwa ajili ya matumizi ya majumbani umeanza katika mikoa  Dar es Salaam ,Lindi na Pwani .

Aidha Haule amewatia moyo wananchi ambao  bado hawajafikiwa na huduma hiyo huku akisema serikakli yao ya awamu ya sita kwa ujumla wake inaendelea kujipanga kuhakikisha wananchi wengi wanafikiwa na gas asilia ukiwemo mkoa wa Dodoma.

Amesema,katika mko huo tayari wameshaanza kufanya stadi ili kufahamu hasa  mahitaji ya huduma itakayohitajika ambapo baada ya stadi kukamilika ndipo shirika litafahamu uhitaji na kuona namna ya kufikisha huduma mkoani humo.

 “Gas asilia inatakiwa ufahamu mahitaji ya eneo husika ndipo upeleke ,hii hatupeleki kama maji au umeme wa kawaida,kwa ujumla stadi inaendelea na pale itakapokamilika tutafahamu kwamba tunahitaji gas kiasi gani ili iweze kuwafikia wakazi wa Dodoma.”amesema Haule na kuongeza kuwa

“Kwa Dodoma bado hatujafika kwa sababu hakuna miundombinu ya gas ambayo imefika Dodoma ,hata hivyo  tayari kuna stadi maalum imefanyika ambayo baada ya kukamilika kwake wakazi wa Dodoma watapata gas asilia ambayo iatakuwa ikisafirishwa kwa njia ya magari  na kutakuwa na kituo ambacho wahitaji wa gas asilia watakuwa wanapata ambayo itasambazwa kutoka kwenye hicho kituo hadi kwa watumiaji kwa huduma mbalimbali.”

Vile vile amesema,hapa nchini kuna ugunduzi wa gas asilia na tayari kuna baadhi ya maeneo wameshaanza kuitumia huku akisema kuwa  serikali bado ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha kwamba na wao wanaanza kutumia gas asilia ambayo itasaidia kuweka mazingira katika hali ya usalama zaidi kwani wananchi wengi watatumia nishati hiyo na kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni ambayo yamekuwa yakisababisha uharibifu mkubwa wa mazingira nchini,

Katika hatua nyingine Haule amesema,pia upo  mradi wa kusambaza  miundommbinu ya kutumia gas asilia kwenye magari na pia kuna baadhi ya viwanda ambavyo tayari vinatumia gas asilia .

Amesema,mpaka sasa tayari kuna jumla  viwanda 52 ambavyo vinatumia gas asilia katika mikoa ya Dar,Pwani na Mtwara .

Kwa mujibu wa Haule TPDC kwa kushirikiana na Gasco ambayo inashughulika na miundombinu ya  gas wameingia mkataba na wananchi wa maeneo ambayo limepita bomba la gas(MKUZA) kwa ajili ya kuhakisha ulinzi wa bomba hilo ambalo limejengwa kutoa Dar es Salaam hadi Mtwara .

Pia amesema, TPDC kwa kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu katika kulinda na kunufaika na uwepo wa gas kwenye maeneo yao ambapo TPDC kwa kutumia Sera yao ya kurudisha kwa jamii wamekuwa wakisaidia wananchi katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika michezo ,masuala ya utawala bora elimu na afya kwa kuweka miundombinu mbalimbali katika maeneo hayo.

“Katika Afya tumekuwa tukishirikiana na wananchi pamoja na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuhakikisha kwamba tunawezesha ujenzi wa zahanati pamoja na kununua vifaa tiba kwenye hizo zahanati..,ambapo kwenye elimu tumekuwa tukishirikiana na halmashauri na wananchi kwa maana ya kata ,vijiji na viongozi wengine kuhakikisha kwamba kwenye sekta ya elimu tunawezesha kujenga madarasa pamoja na kuwapatia madawati na vifaa vingine katika sekta ya elimu.”

Katika masuala ya utawala Bora wamekuwa wakisaidia ujenzi wa ofisi za Serikali za Mitaa kwa maana ya kata na vijiji,kujenga na kuweka samani za ofisi lakini pia wamekuwa wakiandaa mabonza mbalimbali ambayo yanakuwa na dhima tofauti ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kulinda miundombinu,kulinda afya zao lengo kuu ni kujenga ushirikiano na mahusiano mazuri hasa katika kulinda rasiliamli za shirika hilo ipasavyo .



 



Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.