WAZIRI wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu George Simbachawene |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu George Simbachawene ametaja vipaumbele vinavyotarajiwa kutekelezwa na ofisi yake kwa mwaka wa fedha wa 2022/23 ikiwemo mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya.
Vile vile amesema ofisi yake inatarajia kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria mpya ya Menejimenti ya Maafa ya Mwaka 2021.
Simbacghwene ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu utekelezaji wa bajeti ya ofisi hiyo baada ya kupitishwa na Bunge katika mwaka wa fedha wa 2022/23.
Ametaja vipaumbele vingine ni Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi , kujenga uwezo wa kuzuia,kujiandaa na kukabaliana na Maafa kwa Kamati za maafa za ngazi ya mikoa,Halmashauri na serikali za mitaa pamoja na wadau wengine.
Ofisi ya Waziri Mkuu iliidhinishiwa na Bunge kiasi cha shilingi bilioni 101 ili
iweze kutekeleza majukumu yake katika mwaka wa fedha wa 2022/23.
Kuhusu mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya amesema katika Mwaka wa
Fedha wa 2022/23 Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za kulevya
imeidhinishiwa shilingi Bilion 11.9 kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake
ukilinganisha na kiasi cha shilingi Bilion 8.5 kilichoidhinishwa mwaka 2021/22 sawa
na ongezeko la asilimia 28.8.
Amesema ongezeko la bajeti hiyo
litaendelea kuimarisha udhibiti wa biashara na matumizi ya Dawa za kulevya
nchini.
Kuhusu mapambano dhidi ya UKIMWI amesema, Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania
imeidhinishiwa na Bunge shilingi Bilion 14.9 ambapo sh billion 2.9 ni kwa ajili
ya matumizi ya kawaida huku shilingibillion 12 ni kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi ya maendeleo ukilinganisha na bajeti ya shilingi billion 4.3 iliyotengwa mwaka 2021/22 ambapo
ni sawa na ongezeko la asilimia 71.2.
kwa mujibu wa Waziri huyo shughuli zitakazotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/23
ni pamoja na kuratibu upatikanaji wa huduma za VVU na Ukimwi kwenye mikoa ya
kipaumbele ikiwemo Iringa,Kagera,Katavi,Mbeya,Mwa
Aidha kuhusu kukuza Demokrasia nchini amesema,Serikali imekuwa ikifanya jitihada
mbalimbali zenye lengo la kukuza demokrasia nchini,ambapo alisema katika hilo
ili kukamilisha ujenzi wa jingo la Makao Makuu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
siasa jijini Dodoma ambapo kiasi cha sh billion 20.4.
Amesema ili kutekeleza shughuli hizo serikali imeitengea shilingi bilioni 21.9 ofisi
ya Msajili wa Vyama vya Siasa ili iweze kutekeleza majukumu yake na kuongeza
kuwa imeitengea Tume ya Taifa ya uchaguzi sh bilioni
10 kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake.
No comments:
Post a Comment