NA JOYCE KASIKI,DODOMA
RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za maadhimish ya siku ya Mashujaa inayotarajiwa kufanyika Kitaifa mkoani Dodoma.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akikagua maandalizi ya shughuli hiyo kwenye Uwanja wa Mashujaa ,Mkuu wa mkoa wa Dodoma amesema sherehe hizo ambazo hufanyika Julai 25 kila mwaka ,zitaanza mapema asubuhi siku hiyo.
Mtaka ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wote wa mkoa wa Dodoma na wanaoishgi katika mikoa ya jirani kushiriki katika maadhimisho hayo ili kuwaenzi mashujaa hapa nchini.
“Viongozi wa mkoa wa Dodoma tumetembelea eneo hili na tumeona maandalizi yapo vizuri na tumeridhika na tunawaongeza sana kamati ya maandalizi kwa kufanikisha jambo hilo.”amesema Mtaka
Akizungumzi kuhusu changamoto za eneo hilo kuwa katika mazingira yasiyoridhisha,Mtaka amesema,amepata taarifa kwamba eneo hilo ni la jiji huku akiwahakikishia wananchi na Taifa kwa ujumla kwamba kama mkoa utahakikisha eneo hilo linakuwa safi na lenye kuvutia wakati wote.
“Tumesikiliza changamoto za mnara hali ilivyokuwa kabla mpaka eneo kufanyiwa ukarabati, nimeongea na Mkurugenzi wa maadhimisho kwamba ni nani mmiliki wa eneo ili tujue nani mtunzaji..,nimeambiwa mmiliki wa eneo hili ni jiji ,ingawa inaonekana hakukuwa na tafsri sahihi ya umiliki ,lakini sasa nimejua kwamba eneo hili la mashujaa linatuhusu mkoa na jiji,
“Hivyo kwetu sisi mnara wa kumbukumbu za mashujaa ndani ya jiji la Dodoma tutautuza lakini tunatamani eneo kuwa linatembelewa na kuwa eneo la kuvutiwa watu,kwa hiyo ofisi ya mkoa,Ofisi ya Jiji na Ofisi ya maadhimisho tutakutana tukubaline tuone namna gani eno hili litatunzwa vizuri.”amesema Mataka
Amesema,eneo hilo linapaswa kuwa moja ya alama za mkoa wa Dodoma ambapo watu wataenda kupumzika na hata kupiga picha kwa wanaopenda kufanya hivyo.
“Kwa hiyo tupo tayari kuhakikisha kwamba ,eneo hili la Mashujaa linakuwa ni eneo hai kama ambavyo meneo kama haya huko Duniani yanatumika ,kwetu sisi mnara wa kumbukumbu ya mashujaa wetu tutautunza lakini tunatamani liwe ni eneo ambalo litatembelewa,liwe ni eneo ambalo litakuwa ni moja ya alama za mkoa wa Dodoma na kuvutia watu,
“Kwa hiyo ofisi ya mkoa ,ya jiji la Dodoma na Ofisi ya Maadhimisho tutakutaa tukubaliane namna ya kulitunza vizuri eneo hilo,kama kuna haja ya kuweka migahawa midogo,au kutengeneza eneo la kupiga picha lakini tunachukulia kwamba litakuwa ni moja ya alama za mkoa huu,unakuwa mnara wa kuvutia na wakati wote waone wana utambulisho ndani ya mkoa wetu.”amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa
Amesema , kwa mwakani changamoto zote zilizojitokeza mwaka huu zitafanyiwa kazi ili eneo libebe hadhi na heshima ya mashujaa .
Awali Mkurugenzi wa Maadhimiho hayo Bathlomeo Jungu amesema ,hali ya uwanja haikuwa nzuri na hivyo kwa maelekezo ya viongozi walianza shughuli ya marekebisho ya uwanja kwa kutoa nyasi na kumwaga changarawe.
“Eneo la
mnara lilikuwa siyo zuri,lilikuwa chafu na lilikuwa limechoka ,lakini tumewapa
kazi SUMA JKT na wanaendelea na marekebisho mbalimbali na wanakarabati Mwenge
wa juu ya mnara ili kuhakikisha mazingira yote katika eneo hilo yanakaa vizuri
tayari kwa maadhimisho.”amesema Jungu
No comments:
Post a Comment