JKT kuadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwake Julai 10 mwaka huu


MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya miaa 60 tangu kuanzishwa kwa JKT


NA MWANDISHI WETU ,DODOMA

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limeelezea mafanikio yake linapoelekea kutimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake huku likitaja Moja ya mafanikio ni kuchangia katika Pato la Taifa kwa kutoa gawio Serikalini kupitia Shirika lake la uzalishaji Mali la SUMA JKT.

 

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab  Mabele ameyasema hayo leo Machi 3,2023 wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya miaka 60 ya JKT yanayotarajiwa kufanyika Julai 10 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi.

 

Meja Jenerali Mabele amesema SUMA JKT ,kwa nyakati tofauti limeanzisha shughuli mbalimbali za uzalishaji Mali na huduma kupitia Sekta za ujenzi ,uhandisi na ushauri,sekta ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi ,sekta ya viwanda pamoja na sekta ya huduma na biashara lengo likiwa kujiongezea kipato huku akisema hatua hiyo imesaidia kupunguza mzigo wa kibajeti kwa Serikali wa uendeshaji wa shughuli za JKT ,miundombinu ya Makambi ya zamani Serikali imekuwa ikiyaboresha pamoja na kuanziaha Makambi  mapya bila kuathiri majukumu ya msingi.

 

"Jeshi la Wananchi wa Tanzania na  Taifa kwa ujumla linajivunia mafanikio ya JKT katika kutimiza Malengo yake kwa jamii na shughuli zake za kiuchumi ambapo kutokana na umuhimu wake katika Taifa ,JKT limeweka utaratibu wa kujitathimini wapi limetoka,lilipo na linapoelekea  kwa kipindi Cha miaka 10."

 

Vile vile ameelezea  mafanikio mengine ya JKT ni kupitia kilimo mkakati ambacho kilianzishwa kwa ajili ya kuhakikisha JKT linajitosheleza kwa chakula huku akisema ili  kufikia azma ya kujilisha wameanzisha kilimo mkakati ambacho pamoja na changamoto za hali ya hewa hapa nchini ,lakini kwa sasa hawategemei kununua mahindi wala mchele kwa ajili ya kulisha vijana na kwamba  mkakati wao  ni kuhakikisha ifikapo 2024/2025 tunajilisha na kwenye malengo hayo hatuna wasiwasi lengo hilo litafikiwa.

 

Kwa mujibu wa Meja Jenerali Mabele , kuelekea maadhimisho hayo JKT litafanya shughuli za kijamii ikiwemo kuchangia damu ,kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ikiwemo hospitali ,upandaji wa  miti ili kuendelea kuifanya Dodoma ya kijani na kutoa msaada wa kibinadamu kwa wahitaji .

 

Aidha Meja Jenerali Mabele amesema pamoja na utekelezaji wa shughuli zote hizo lakini pia JKT bado limeendelea na majukumu yake ya msingi ya malezi ya vijana ,uzalishaji mali na Ulinzi limekuwa likifanya maboresho mbalimbali ili kuendana na wakati pamoja na mabadiliko ya satansi na Teknolojia

 

Kwa upande wake Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT Brigedia Hassan Mabena amesema Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikiitumia Taasisi hiyo kuhakikisha vijana wanapata uzalendo,ukakamavu,mafunzo ya ujasiriamali,mafunzo ya ufundi stadi ambapo vyote kwa pamoja vinakwenda kuwasaidia wao katika kujiajiri na kuendesha maisha yao.

 

Naye ,Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho hayo Kanali George Kazaula amesema JKT limewaalika wadau mbalimbali kuelekea maadhimisho hayo kwa lengo la kuhakikisha yanafanyika kama yalivyopangwa.

 

Share:

Dkt.Ndumbaro amewataka viongozi wa taasisi za utoaji haki kushirikiana katika kuondoa vikwazo vinavyokwamisha utekelezaji wa sheria ya watoa taarifa

 

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA DKT.DAMAS NDUMBARO



NA OKULY JULIUS ,DODOMA

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt.Damas Ndumbaro ,amewataka viongozi wa taasisi za utoaji haki kushirikiana katika kuondoa vikwazo vinavyokwamisha utekelezaji thabiti wa Sheria ya watoa Taarifa na Ulinzi wa Mashahidi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Dkt.Ndumbaro ameyasema hayo leo Februari 28,2023 Jijini Dodoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kanuni za watoa taarifa na Ulinzi wa Mashahidi ,ambapo amesema kuwa taarifa zinaonesha kuwa utayari wa wananchi kutoa taarifa umeongezeka na walio wengi wako tayari kushiriki katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kufika katika vyombo vya sheria.

Amesema kuwa watanzania wakishiriki kwa pamoja katika kufichua maovu yakiwemo yanayosababisha hasara kwa taifa utasaidia kukuza uchumi na kuweka mazingira wezeshi kwa uwekezaji.

4I6A6210.JPG

"Ili tufikie malengo yaliyokusudiwa ya kuhakikisha tunafichua kila aina ya maovu yanayotokea ikiwemo ufisadi,ukiukwaji wa haki za binadamu na matumizi mabaya ya madaraka na mengine mengi yaweze kuripotiwa bila woga kwa maslahi mapana ya nchi yetu,"

Na kuongeza kuwa "Niwaombe tuendelee kutoa elimu ya kisheria kwa umma wa watanzania kuhusiana na sheria na kanuni tajwa ili wawe na uelewa na wajue umuhimu wa kuwafichua wahalifu wa makosa mbalimbali yanayotendeka katika jamii yetu ili mwisho wa siku matukio ya kiuhalifu yapungue na na hatimaye kuisha kabisa,"amesema Dkt.Ndumbaro

4I6A6242.JPG

Pia Dkt.Ndumbaro amewataka wananchi kutohofia kujitokeza kutoa taarifa za uhalifu na matendo ya aina zote yanayofanywa kinyume cha sheria, kwani taarifa hizo zitakuwa siri na zitafanyiwa kazi bila ya kuwataja watoa taarifa , pia mashahidi wanapotakiwa kufika mahakamani wasiogope kwani Kanuni hizo zinaweka mfumo wa kuwalinda ambao unaeleza masharti na namna za ulinzi huo.

"Kanuni hizi zinalenga kurahisisha utekelezaji wa Sheria na kuongeza ufanisi katika utekelezaji na kufikiwa kwa madhumuni ya Sheria. Sambamba na hilo, Kanuni hizi zitasaidia kuwapatia ulinzi wa kisheria wale wote wanaotoa taarifa za uhalifu wa makosa ya aina mbalimbali na hivyo kuwaongezea imani na usalama wao na hivyo kurahisha uendeshaji wa mashtaka,"amesisitiza Dkt.Ndumbaro

4I6A6230.JPG

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na ufuatiliaji Haki Kharist Luanda amesema kuwa kuzinduliwa kwa kanuni hizo inafungua milango kwa wananchi kuanza kutoa taarifa mbalimbali kwa kujiamini kwani kanuni hizo zimebainisha namna watoa taarifa na mashahidi watakavyopatiwa ulinzi.

"Kanuni hizi ni muhimu sana kwani zinamuhakikishia ulinzi mtoa taarifa na shahidi na kumtengenezea uhuru hata wakati wa kutoa ushahidi mahakamani kwa sababu kanuni hizi zimeshamuhakikishia usalama,"amesema Luanda

4I6A6061.JPG

Kanuni hizo za Watoa Taarifa na Ulinzi wa Mashahidi zimekuja baada ya Serikali, mwaka 2016 kuanza kutekeleza Sheria ya Watoa Taarifa na Ulinzi wa Mashahidi ya mwaka, 2016 (The Whistleblower and Witness Protection Act. 2016 ,sheria hiyo ikiwa na lengo la kuimarisha misingi ya utoaji haki jinai na kukuza utawala bora na mapambano dhidi ya uhalifu nchini.

Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.